0
Tarehe 31 Oktoba 2017 Alexander Mnyeti alikabidhiwa rasmi kiti cha mkuu wa mkoa wa Manyara baada ya kapandishwa cheo na Rais Magufuli kutoka ukuu wa wilaya ya Arumeru na kuchukua nafasi ya Dr.Joel Nkaya Bendera aliestaafu ajira serikalini.

Dr. Bendera atakumbukwa kwa utendaji kazi wake mzuri katika nafasi alizowahi kupitia huku akikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi katika mkoa wa Manyara na kufanikiwa kuipunguza kwa kiwango kikubwa japo bado migogoro hiyo ipo.

Aliyekabidhiwa nafasi hiyo Alexander Mnyeti ameshaanza kazi rasmi katika mkoa wa Manyara na ziara yake ya kwanza ameanza leo katika wilaya ya Simanjiro katika mji mdogo wa Mererani panapojengwa ukuta kwenye vitalu vya machimbo.
Image result for ukuta mererani kujengwa
Eneo la Mererani panapojengwa ukuta huo.

Ujenzi wa ukuta huo ni agizo alilolitoa Rais John Magufuli akiwa  kwenye sherehe ya ufunguzi wa barabara ya Kia - Mererani iliyofanyika katika eneo la Mererani, kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kujenga ukuta wa kuzunguka vitalu vya kuanzia Block A hadi D vyenye madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani, Wilaya ya Simanjiro ili kudhibiti uchimbaji na biashara ya madini hayo.

Rais Magufuli alisema pamoja na kujenga ukuta huo haraka iwezekanavyo, soko la Tanzanite litapaswa kuwa katika eneo hilo, Tanzanite yote itapita kupitia lango moja na ameitaka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kushiriki katika ununuzi wa Tanzanite.

Mnyeti ametoka wilaya ya Arumeru alipokuwa akitumika kama Mkuu wa wilaya ila itakumbukwa kuwa aliingia mgogoro na wana habari mkoani Arusha kwa kujaribu kuminya kazi za waandishi wa habari na kulazimika wana habari kumfungia kwa kutomwandika kwa lolote atakalolifanya mkuu huyo wa wilaya kwa kipindi cha miezi sita kuanzia february mwishoni hadi September 2017.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top