Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Mwigulu Nchemba amewakosoa upinzani
kutumia tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki
Tundu Lissu kama ajenda katika kampeni za uchaguzi wa marudio na kusema
kwamba chama hicho kimefilisika.
Akiwa
Masasi katika kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa tiketi ya CCM,
Dkt Nchemba amesema kwamba kitendo hicho cha Chadema kufanya kila mahali
tukio la Lissu kama ndiyo ajenda atakwenda kuwaambia wakazi wa Singida
wawaangalie vizuri watu hao.
"Mimi
nitaenda kuwaambia wana Singida kwamba tuwaangalie vizuri hawa watu.
Wao ni mwenzao kwenye Chama sisi ni ndugu yetu na tunatoka sehemu moja.
Inawezekanaje wawe wanafurahia tukio hilo? Kama kuna kitu walikuwa
wanataka kitokee ili warushe maneno kwa serikali" amesema Dkt Nchemba.
Aidha
akiendelea Nchemba amesema Chadema wanamuona kama Lissu mtaji ndiyo
maana hata polisi walipomtaka dereva wake ili kuweza kumhoji wameamua
kukaa naye huko.
Pamoja
na hayo Nchemba amewata watu wakapige kura bila kuhofia fujo zinazoweza
kufanywa na wanachadema kwani serikali ipo kwa ajili ya kusimamia
sheria.
"Wamezoea
kufanya fujo. Nendeni mkapige kura akitokea mtu atakayethubutu
kukughasi wewe mkariri sura alafu sisi tutamfundisha ustaarabu wa vyama
vingi. Anayefanya fujo atakutana na mkono wa sheria. Na uzuri vijana
wangu wapo hapa atakayethubutu kufanya fujo, Muwaonyeshe kwamba mmepitia
mafunzo" Nchemba
Hata
hivyo Nchemba amewataka wananchi hao kuichagua CCM kwa kazi nzuri
inayofanya na kuwaamba kuuchagua upinzani wakitegemea itashinda ni sawa
na kujeruhi nafsi.
Post a Comment
karibu kwa maoni