Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameamuru ng'ombe waliobaki hai kati ya
692 waliokufa katika Pori la Akiba la Rukwa/Lwafi, waliokuwa
wameshikiliwa warudishiwe kwa wamiliki wa mifugo hiyo.
Akiwa
katika ziara yake Mh. Mpina amelazimika kutoa maamuzi hayo baada ya
kukuta mizoga 692 ya ng’ombe ikiwa imetapakaa katika Pori hilo ambapo
imedaiwa kwamba ng'ombe hao walikufa kwa kukosa mahitaji muhimu.
Waziri
Mpina ameshangazwa kuona mizoga mingi kiasi hicho huku mifugo hai
ikiishi zizi moja na iliyokufa, huku kukiwa na harufu mbaya
Imeelezwa
kwamba mazingira hayo yamechangia kasi ya maambukizi ya magonjwa
nyemelezi kuwa kubwa zaidi na kupelekea ongezeko la vifo kwa mifugo
hiyo.
Hata
hivyo baada ya kushudia Mizoga hiyo, Mh. Mpina amepokea taarifa ya
Mkoa, Wahifadhi, Chama cha Wafugaji na wamiliki wa mifugo hiyo na
kupitia nyaraka mbalimbali, ilibainika kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya
Sumbawanga, ilitoa amri ya ng’ombe hao kukabidhiwa kwa wenyewe tangu
Julai 27, mwaka jana.
Mifugo hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika hifadhi hiyo tangu mwezi machi mwaka jana.
Post a Comment
karibu kwa maoni