0
Jack CorkKiungo wa kati wa Burnley Jack Cork ameitwa kujiunga na kikosi cha England kinachojiandaa kwa mechi za kirafiki dhidi ya Ujerumani na Brazil.
Raheem Sterling, Fabian Delph na Jordan Henderson walijiondoa kutoka kwenye kikosi cha Gareth Southgate Jumanne baada ya wachezaji watatu wa Tottenham Harry Kane, Dele Alli na Harry Winks pia kujiondoa.
Cork, 28, bado hajachezea timu ya taifa lake mechi hata moja.
Alijiunga na Burnley kutoka Swansea mwezi Julai na amecheza kila dakika mechi ambazo Burnley wamecheza Ligi ya Premia msimu huu kufikia sasa.
"Nina furaha sana, nafurahi sana," amesema.
Cork alikuwa amewakilisha England katika vikosi vya wachezaji wa chini ya miaka 16 na chini ya miaka 21 na pia aliwakilisha Uingereza katika Michezo ya Olimpiki ya London akichezea Southampton wakati huo.
Beki wa Chelsea Gary Cahill pia amejiunga na kikosi cha England, baada ya kuchunguzwa na matabibu wa klabu yake kutokana na wasiwasi wa jeraha.
England watacheza dhidi ya Ujerumani uwanjani Wembley Ijumaa na kisha dhidi ya Brazil uwanja uo huo mnamo 14 Novemba.

Kikosi cha England

Walinda lango: Jack Butland (Stoke City), Joe Hart (West Ham - kwa mkopo kutoka Manchester City), Jordan Pickford (Everton).
Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Joe Gomez (Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Michael Keane (Everton), Harry Maguire (Leicester), Danny Rose (Tottenham), John Stones (Manchester City), Kieran Trippier (Tottenham), Kyle Walker (Manchester City).
Viungo wa kati: Eric Dier (Tottenham), Jesse Lingard (Manchester United), Jake Livermore (West Brom), Ruben Loftus-Cheek (Crystal Palace - loan from Chelsea), Ashley Young (Manchester United), Jack Cork (Burnley).
Washambuliaji: Tammy Abraham (Swansea - loan from Chelsea), Marcus Rashford (Manchester United), Jamie Vardy (Leicester).

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top