0
Raia wa Zimbabwe walivyofurahia kuapishwa kwa rais mpyaRais mpya wa Zimbabwe amesema kuwa jukumu lake halitatekelezwa kupitia hutuba.
Lazima nianze kazi....
Tutaanza kazi kwa haraka kutoka pale alipowachia aliyekuwa rais wetu Robert Mugabe.
Hatuwezi kubadili yaliopita, kuna mengi ambayo tunaweza kufanya kwa sasa ili kulipatia taifa letu mwelekeo mpya.
Hatuwezi kukubali kuwa watumwa wa yaliopita.
Amesema kuwa mabadiliko ya umiliki wa ardhi yalifanyika na hayawezi kubadilishwa kwa kuwa huo utakuwa ukiukaji mkuu wa upiganiaji wa Uhuru.
Lakini rais huo mpya ameahidi kuwalipa wakulima waliopoteza mashamba yao katika sera tata iliotekelezwa na utawala wa rais MUgabe.
Emmerson Mnangagwa, kwa jina la utani The the crocodile", ameanza hotuba yake kama rais wa Zimbabwe.
''Nahisi furaha sana kwa uamuzi wa chama cha Zanu PF kunialika kuhudumia taifa letu la Zimbabwe kama rais na kamanda mkuu wa majeshi kuanzia leo''.
''Sina ujuzi wa kazi hii lakini nitawahudumia wananchi wote bila upendeleo wa rangi ama kabil''a. Amemsifu Robert Mugabe kwa kupiginia uhuru huku akisema kuwa alichukua uongozi wakati mgumu .
Amesema kuwa licha ya makosa yaliofanywa na Mugabe ni muhimu kukubali na kutambua mchango wake kuhusu ujenzi wa taifa. ''Kwangu mie bado ni rafiki mkubwa''.

Wakuu wa jeshi wampigia saluti Mnangagwa

Wakuu wa jeshi sasa wanampigia saluti kamanda mpya wa jeshi na kusalimiana kwa mkono.
Ni Jeshi lililochukua jukumu kuu siku 10 zilizopita ambazo zilisababisha kujiuzulu kwa Robert Mugabe.
Bwana Mnangagwa amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na makamanda wakati alipofurushwa na rais Mugabe kama naibu wake.
Alisema kuwa kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua ndio sababu akaondoka nchini humo na kurudi siku ya Jumatano baada ya Mugabe kujiuzulu.
Akaunti moja ya mtandao wa twitter unaochunguza vyombo vya habari nchini Zimbabwe imesema kuwa rais mpya anakagua gwaride la heshima kwa kutembea huku aliyekuwa rais wa zamani Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 alikuwa akifanya hivyo kwa kutumia gari. 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top