Sekta
binafsi
inatakiwa kuhakikisha fedha inazokopa kwa ajili ya uwekezaji au
biashara zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze kurejesha
mikopo yao kwa
wakati na hivyo kupunguza ongezeko la Mikopo Chechefu (NPL).
Waziri
wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) aliyasema hayo wakati wa
mkutano wa
uwekezaji uliojumuisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
ulioangazia changamoto ya upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi kutoka
taasisi za fedha katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo, katika mikutano
ya kipupwe inayoendelea mjini
Washngton DC, Marekani.
Amesema
kuwa, licha
ya kuwepo kwa wakopaji wasiorejesha mikopo kwa wakati pia mwenendo mzima
wa baadhi ya taasisi za fedha zikiwemo benki kutozingatia kanuni na
taratibu za ukopeshaji, jambo linalosababisha kuongezeka kwa mikopo
chechefu.
Akizungumzia kuhusu
kupungua kwa mikopo kwenye Sekta binafsi katika Jumuiya hiyo, Waziri Mpango amewataka
wananchi watambue kuwa ziko changamoto ambazo zinatokana na mahusiano ya
kiuchumi ya ulimwengu yanayosababisha kupungua kwa bidhaa ambazo zinauzwa nje ya nchi hivyo kuathiri sekta binafsi.
Amesema
matokeo kupungua kwa biashara ama mauzo nje ya nchi kumewafanya
wafanyabiashara kupunguza uwezo wao wa kurejesha mikopo waliyokopa
katika benki, hivyo wananchi wasione kama ni tatizo la jumuiya hiyo tu
bali
lazima kuunganisha kinachotokea na
mwenendo wa kibiashara kimataifa.
Sababu nyingine ni
kupungua kwa fedha zilizokuwa zinaingia katika mfumo wa kibajeti miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kutoka kwa nchi
wahisani na hivyo kuzifanya nchi kukopa kwenye taasisi za fedha za ndani ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
“
Katika
majadiliano haya tumekubaliana kuendelea kuzungumza na sekta binafsi na
kushughulikia matatizo yanayowakumba hasa suala la malipo ya madai yao
mbalimbali ili waweze kulipwa haraka na kuondoa vikwazo katika mitaji yao
ya biashara ili waweze kurejesha mikopo waliyokopa katika benki.” alisema Dkt.
Mpango.
Kwa upande wake Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga,
ambaye alishiriki majadiliano hayo ya uwekezaji alisema kuwa, sekta binafsi
ina umuhimu mkubwa katika kukuza maendeleo ya nchi kupitia uwekezaji wao.
“Nchi
za
Afrika Mashariki zisipokuwa na uwekezaji mkubwa kupitia sekta binafsi,
benki zitakosa utayari wa kutoa mikopo kwa sekta hizo kwa kuwa na
wasiwasi wa
urejeshwaji wa mikopo hiyo”, alieleza Gavana Luoga.
Amesema nchini Tanzania
benki binafsi zimeanza kushiriki katika
uwekezaji kwenye sekta binafsi, hata hivyo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inafanya
majadiliano na benki hizo ili kuangalia jinsi zinavyoweza kuongeza uwekezaji
kwa kutoa mikopo huku jambo linalotakiwa kutiliwa mkazo ni ushirikiano na sekta
hizo ili ziweze kukopesheka suala ambalo Serikali imekuwa ikilijadili pia na
nchi nyingine na kuwa na mafanikio chanya.
Post a Comment
karibu kwa maoni