Kikosi cha timu ya BABATI MASHUJAA[ BM SC]. |
Mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Babati [BDFA] Gerald Mtui amesema ligi inaendelea vizuri na imebaki michezo nane ili kukamilisha michuano hiyo inayoshirikisha timu sita.
Ligi hiyo imeendelea tena jana na kuwakutanisha BM SC ya mjini Babati dhidi ya KARIAKOO ya Gidas mchezo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute Bm Sc wakianza kupata mabao 2 kipindi cha kwanza na kuwaacha Kariakoo wakiwa na mawazo namna ya kurudisha mabao hayo.
Kipindi cha pili kilianza huku timu zote mbili zikikamiana vikali kupata mabao lakini Bm Sc wakawazidi nguvu wenzao hao wa Kariakoo na kumaliza mchezo BM SC 3-KARIAKOO.
Kwa matokeo hayo Bm Sc anaongoza ligi hiyo kwa alama 10,Mrara Fc alama 4,Ngurumo anaecheza leo na Vijana Sc wenye alama 1 yeye anazo alama 3,Kariakoo alama 3 na Town Boys alama 1.
Akizungumza na WALTER HABARI kocha wa Bm Sc James anasema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaongoza ligi mpaka mwisho na kuchukua ubingwa na hatimaye kushiriki ligi ya Mkoa.
Post a Comment
karibu kwa maoni