0
Na Gharib Mzinga
Kutolewa kwa Kili stars Lawama zimeelekezwa kwa Ammy ninje !, Sawa, kama inaonekana yeye ndio tatizo, lakini watanzania wasisahau kua Ninje hakuanza yeye kulaumiwa, Kila mashndano Tanzania huwa haifanyi vyema na lawama huenda kwa walimu, Ina maana Tff haijitambui? Haijui walimu bora? Tunadhani tff ikimuajili Pep Guardiola ndio itafanya vizuri? Nchi nyingi za Afrika magharibi na kaskazini ndizo zinazotawala Soka la Afrika na hata kimataifa huwakilisha wao pia, Nchi zile zina vipaji vingi sana, Wachezaji hubadirika kila mashindano, kwakua wanaandaliwa wengi, Sitaki kuzungumzia sana Afrika magharibi na kaskazini huo sio mfano bora sana.
Huu ukanda wa Afrika mashariki (cecafa) na Afrika kusini (cosafa) Nchi nyingi hazina  maendeleo kisoka tangu hazijapata Uhuru mpaka wakati huu, Lakini kuna baadhi ya Nchi chache zimeangalia mbali na zinapata mafanikio kisoka, nchi kama Zambia, Zimbabwe, Congo, Afrika kusini, Uganda na msumbiji kidogo, Mataifa haya yameamua kujitofautisha na mengine  katika kuendana na kasi ya ulimwengu wa Soka inavyokwenda. Zambia ina vituo vingi vya kukuzia vijana kuanzia umri wa miaka 6, lakini pia wana vituo vikubwa vinne Breakthrough Chiparamba sports Academy, Ambassador football Academy, Faz  football Association, na European football academy, hivi vituo ndio vinazalisha wachezaji wapambanaji wengi wa kila umri ambao wanafanya vizuri katika mashindano yote. kipindi Tanzania inapeleka  akina John boco, kelvin Yondani, Erasto Nyoni, katika cosafa Zambia ilipeleka vijana wapya kutoka vilabu 9 vya ndani na hakuna mchezaji aliyetoka Zesco na Zanaco ambazo ndio timu kubwa zaidi.
Zimbabwe. hawa wameamua kuwekeza kwa walimu wengi wa kigeni na kuanzisha mpango maalum wa maendeleo ya Soka kupitia vituo vya kukuzia vijana wapambanaji, Zimbabwe football development Academy grassroot. Mpango huu umeisogeza mbele taifa hilo. kupitia mikakati ya aina hii Zimbabwe imepiga hatua kubwa kwa kuandaa wachezaji wengi wanaosakata kabumbu maeneo yote ya kusini mwa Afrika na ulaya, khama billiati, Tendai Ndoro, Devon Chafa, knowledge musona ni mfano mzuri wa mastaa wao, kipindi tanzania inaweka kumbukumbu ya mwaka 1980 kua ni mwaka wa kihistoria, Zimbabwe wameshiriki Afcon ya mwisho kule Gabon, Afrika kusini taifa hili lina miundo mbinu mingi na Bora, lakini udongo wake hauna Rutuba ya kuzalisha wachezaji wazuri wengi, kwa kuijua hilo wameamua kuwekeza katika Soka la vijana, katika michuano ya cosafa hawakuona tatizo kuingiza wachezaji wenye umri mdogo ili kuwajenga Kama vile Innocent Maela, Baolefa Pule, Bruce Bruma, Thendo Mukumela na wengine, hao ni zao la vituo vya vijana Afrika kusini licha ya vituo vya shirikisho vya kukuzia vijana bado vilabu vinazalisha wachezaji wengi ambao husaidia taifa  ndio maana wanamtumia Siphiwe tshabalala kama mkongwe ambae atacheza michezo michache isiyo ya kishindani huku Tanzania ikiamini kwa Kelvin Yondani kwa asilimia zote.
Msumbiji, wameanza kuweka mipango ya maendeleo kupitia kuajili walimu wengi kutoka Italy, pia wameanzisha kituo kikubwa cha kukuzia vijana Avrio Mozambique Football Association. Kituo hiko na vingine vidogo ndivyo chachu ya maendeleo ya kisoka msumbiji, Nchi hii ilipata uhuru mwaka 1975, mchezo wao wa kwanza wa kimataifa walicheza dhidi ya tanzania mwaka 1977 na msumbiji walipigwa Goli 2-1 kwao maputo, kama ulikua aufahamu msumbiji imeshashiriki Afcon Mara nne  1986-1996-1998 na 2010, Tanzania imepata Uhuru mwaka 1961 imeshiriki Afcon Mara moja tu 1980.
Uganda, hawa wameamua kuiongoza Afrika Mashariki lakini nchi zenyewe hazitaki kufata njia, Uganda ndio Nchi yenye vituo vingi zaidi vya kukuzia vijana tangu ngazi ya msingi, kuliko Nchi yoyote ya Afrika Mashariki na kati. Wana vituo zaidi ya 90 ambavyo vimesajiliwa na vinapata haki zote, vituo hivyo kama vile Palisa youth, Namakwekwe youth, Budaka academy, Proline soccer academy na vingine vingi, Tff hamuoni hili? Timu ya taifa ya Uganda inayoshiriki Cecafa kwa sasa ni vijana wapya mbali na ile timu kubwa ya taifa. Nilitarajia kuona Serengeti boys katika michuano hii.
Kushindwa kufanya vizuri hata katika chalenji ni Aibu kubwa, Tanzania ndio nchi ya kwanza kupata Uhuru katika cecafa, Tanzania ina idadi kubwa ya watu katika cecafa, Tanzania miongoni mwa mataifa yenye miundombinu mingi katika cecafa. Tuandae vituo vya wachezaji wapambanaji.
Ammy ninje hastaili lawama hizo, Tunajua tunapokosea hakuna miujiza katika Soka.
Shirikisho la Soka msifumbe macho, mzigo huu wa lawama unawahusu kwa asilimia zaidi ya 80.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top