0


Image result for joel benderaKOCHA aliyeiwezesha Tanzania kufuzu fainali pekee za Kombe la soka la Mataifa ya Afrika (AFCON), Joel Nkaya Bendera amefariki dunia jioni ya leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Bendera amefariki ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu kustaafu utumishi wa serikali akiwa mkuu wa mkoa wa Manyara ambapo alimpisha Alexender Mnyeti
Msemaji wa hospital ya Muhimbili, Aminieli Eligaisha amethibitisha  kufariki kwa Bendera aliyewahi pia kuwa Naibu Waziri wa Michezo wakati wa Serikali ya awamu ya nne, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top