Mbunge
wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu ametoa msimamo unaotofautiana
na ule uliotolewa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kuhusu ushiriki katika uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani.
Ukawa
wamesema kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haitaahirisha uchaguzi
huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani ili kuruhusu majadiliano,
hawatashiriki uchaguzi huo. Lakini Komu amesema kufanya hivyo ni kosa
kubwa linaloweza kuwaathiri katika chaguzi zijazo.
Viongozi
wa Ukawa unaoundwa na Chadema, Chauma, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF
waliitaka Nec kuahirisha uchaguzi huo katika majimbo ya Singida
Kaskazini, Longido, Songea Mjini na ule wa kata sita ili wadau wapate
nafasi ya kujadili kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mdogo kwenye
kata 43 vinginevyo hawatashiriki.
Viongozi
wa Ukawa; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwenyekiti wa Baraza
Kuu la CUF, Julius Mtatiro; Kaimu Katibu wa Chauma, Eugene Kabendera na
Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Danda Juju walitoa msimamo huo juzi lakini
jana Komu akizungumza kuhusu uamuzi huo wa Ukawa alisema uamuzi ni
halali kwa kuwa umepitia vikao halali, lakini unaweza kujadiliwa.
“Usahihi
ni kitu kingine. Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano,
kwenye vita unapopigana unaonyesha wapi unakosea na kujisahihisha,”
alisema mkurugenzi huyo wa fedha wa zamani Chadema.
“Hata
hizo kata 43 hatukuonewa kote ndiyo maana tulishinda kata moja
tuliyojipanga vizuri, kikubwa tunapaswa kujenga uwezo wetu na kupambana…
kama tutasusia je, tumejipangaje kuhakikisha hicho tunachokipigania
tutakipata?” alihoji.
Mbunge huyo alisema uamuzi huo unazua maswali mengi kwani CCM itapita katika majimbo yote bila kupingwa...
“Watapata
jukwaa la kueleza mambo yao sisi hatutapata, lakini je, kama huu
hatutashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa mwaka 2020
tutashiriki au la, haya ndiyo maswali yanayohitaji majibu.”
Juzi,
Mbowe alisema kulikuwa na kasoro nyingi kwenye uchaguzi wa kata 43
ambazo zinahitaji kurekebishwa, lakini mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC,
Ramadhan Kailima katika taarifa yake aliyoitoa jana alisema chama cha
siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe.
“Ikitokea
vyama vikasusa vyote kushiriki kwenye uchaguzi hapo ndipo unaweza
kuahirishwa kwa kuwa hakutakuwa na mgombea,” alisema Kailima.
Post a Comment
karibu kwa maoni