Polisi
mkoani Arusha imesema imeanza uchunguzi wa kina wa kuwasaka washukiwa,
huku ikichunguza silaha ya Nassari aina ya shotgun, ikisema tukio hilo
lina utata kutokana na mazingira lilivyotokea.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Charles Mkumbo amesema kuwa wameanza uchunguzi wa kina ili kubaini endapo kulikuwa na tukio au la.
“Tunaifanyia uchunguzi bunduki yake, tunataka kujiridhisha endapo kulikuwa na tukio au la,” alisema Mkumbo.
Hata
hivyo, kamanda huyo alisema msako unaendelea ili kuwabaini washukiwa na
kwamba hawajapata maganda ya risasi zinazodaiwa kutumika katika uvamizi
huo.
Juzi
Nassari aliwaambia waandishi wa habari kuwa nusu saa baada ya kuwasili
nyumbani kwake alisikia hali isiyo ya kawaida ndani ya uzio wa nyumba na
baadaye kulisikika milio ya risasi. Alisema mbwa wake aliyekuwa
akibweka alinyamaza, hali iliyomfanya achukue silaha yake kujihami.
“Nilipiga
risasi tano, kisha kukawa kimya nikaenda kuwaamsha vijana wanaonisaidia
hapa nyumbani kuwaeleza tukio lililotokea kisha nikaondoka.”
Alisema
waliofanya tukio hilo hawakujua kama ana silaha kwa sababu mwaka 2014
wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, bastola yake ilichukuliwa na
polisi na hadi leo haijarudishwa, hivyo kuwa na silaha nyingine
kulimsaidia kujibu mapigo.
Katika
tukio hilo, Nassari alisema aliwajibu watu hao kwa kupiga risasi tano
hewani huku wenyewe wakipiga 12 na moja ilimpata mbwa wake ambaye
alimzika juzi katika maeneo ya nyumba anayoishi.
Hivi
karibuni mbunge huyo aliwasilisha makao makuu ya Takukuru ushahidi wa
CD aliodai kuwa unawahusisha madiwani wa Chadema mkoani Arusha
kushawishiwa kuhamia chama tawala.
Post a Comment
karibu kwa maoni