0
Sehemu ya Mji wa Kigoma.SERIKALI imesema itavunja mkataba na kampuni ya Saxon Building Contractor, iwapo haitakamilisha ndani ya miezi mitatu mradi wa ujenzi wa gati ya kuegesha meli katika Kijiji cha Sibwesa Tarafa ya Buhingu wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino, Atashasta Nditiye alikerwa na kuchelewa kwa mradi huo na kuipa miezi mitatu imemaliza, kinyume chake serikali itavunja mkataba na kampuni hiyo.
Akikagua maendeleo ya mradi huo, alisema kuwa anakerwa na kitendo cha kampuni hiyo, kushindwa kutekeleza mradi huo kulingana na mkataba uliowekwa na badala yake imekuwa ikitoa sababu zisizo na msingi.
Nditiye alisema kuwa kampuni hiyo ilipaswa kumalizika mradi huo Desemba 30 mwaka 2016, lakini mwaka mzima umepita bado kampuni hiyo haioneshi jitihada zozote za kumaliza mradi huo.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa kitendo cha kampuni hiyo, kuchelewa kumaliza mradi huku ikiwa imelipwa kiasi kikubwa cha fedha, kinatokana na uzembe wa uongozi wa Mamlaka ya Bandari makao makuu, kushindwa kutembelea na kukagua mradi huo.
Alisema uongozi wa mamlaka hiyo, ulikuwa ukilipa fedha kwa kampuni hiyo, bila kuona hatua za utekelezaji zilizofikiwa. Awali akitoa taarifa kwa waziri, Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Cyprian Simon kutoka kampuni ya Saxon Buidling Contractor alisema kuwa mradi huo unatarajia kugharimu Sh bilioni 3.4 na kwamba ulipaswa kukamilika Desemba 30 mwaka jana, lakini miundombinu mibovu ya usafiri na vifaa vya ujenzi, vimechangia kutokamilika kwa wakati kwa mradi huo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top