Jeshi
la Polisi mkoa wa Mara linawashikilia watu zaidi ya 40, wakazi wa
Kijiji cha Mikomariro wilayani Bunda kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili
sababu ikitajwa kuwa ni mgogoro wa mpaka wa shamba.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed amethibitisha kukamatwa kwa watu
hao huku akiongeza kuwa Jeshi lake bado linawasaka watu wengine
waliohusika na tukio la mauaji ya watu wawili wakazi wa Kijiji cha
Remng'orori wilayani Serengeti.
Aidha
kamanda Jafari amebainisha kuwa waliokamatwa ni wale walioshiriki yowe
iliyosababisha mauaji ya watu wawili kwa kuwakata kwa mapanga kwa sababu
ya ugomvi wa mipaka ya mashamba.
Amesema
kuwa chanzo cha mgogoro huo ni mpaka wa wilaya za Bunda, Serengeti na
Butiama ambao unahusisha eneo la ekari 3,535 ambapo Wegesa Gikene na
Nyamhanga Gembo wakazi wa Kijiji cha Remng'orori waliuawa kwa kukatwa na
mapanga wakati wakiwa shambani.
Post a Comment
karibu kwa maoni