0
Halmashauri tano zilizo chini ya vyama vinavyounda Ukawa zipo hatarini kunyakuliwa na Chama cha Mapinduzi kutokana na wimbi la madiwani kujivua uanachama na kuhamia CCM huku wakidai wanaenda kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Hamahama hiyo imeonekana kukiathiri zaidi Chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema ambacho ndicho kilishinda kata nyingi za udiwani kulinganisha na vyama vingine vya upinzani.

Halmashauri hizo ambazo sasa zinaonekana kukielemea chama hicho ni pamoja na Arusha, Arumeru, Iringa na Siha ambazo madiwani wake wamekuwa wakijivua uanachama kadri siku zinavyoenda.

Tangu kuanza kwa hamahama hizo CCM wameonakana kunufaika zaidi kulinganisha na Chadema kutokana na kushinda chaguzi hizo hata pale zinaporudiwa na hivyo kuongeza idadi kubwa ya madiwani katika mikoa ambayo Chadema ilikuwa inaongoza.

Tayari madiwani 21 wamekwisha kuhama Chadema na kujiunga na CCM huku wimbi hilo likionekana kuzidi kushika kasi.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema bara, John Mnyika alisema CCM haitoweza kuzichukua halmashauri hizo kwa kuwa wameshaanza mikakati ya kudhibiti mbinu chafu zinazotumiwa na CCM katika kuwachukua madiwani wao.

" Sisi tunachokipigania ni kuleta maendeleo kwa wananchi wetu bila kujali itikadi zao za kisiasa na wala suala la hamahama linalofanywa na madiwani na viongozi wengine wa siasa halitusumbui kichwa na wala hatuangaiki nalo," Alisema Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Ngamela Lubinga.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top