Wambura
amesema kamati baada ya kupokea ripoti ya mechi namba 103 kati ya
wenyeji Majimaji FC dhidi ya Azam FC timu ya Azam FC iligoma kuingia
kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa
kanuni za ligi kuu.
Mbali
na faini hiyo klabu hiyo pia imetakiwa kuwasilisha ushahidi kuhusu
malalamiko yake kwenye mchezo huo ambapo ilidai kutoingia kwenye vyumba
hivyo kwasababu vilikuwa vimepuliziwa dawa ambayo ilikuwa inatoa harufu
kali.
Kwa
upande mwingine mwamuzi wa wa mchezo kati ya Azam Fc na Yanga Sc Israel Nkongo ameundiwa kamati ya watu watatu kwaajili ya kuchunguza
maamuzi yake kwenye mchezo namba 100 kati ya Tanzania Prisons dhidi ya
Mbeya City kutokana na kuwepo kwa utata katika maamuzi yake.
Hata
hivyo Azam FC Jumatatno iliyopita waliwasilisha barua TFF wakiomba
kubadilishwa mwamuzi ili achezeshe mwingine badala ya Israel Nkongo
lakini ombi lao limetupiliwa mbali.
Post a Comment
karibu kwa maoni