Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amefunguka na kukanusha taarifa
alizotoa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Siha, Dkt Mollel kuwa aliamua
kuhama CHADEMA na kwenda CCM kwa kuwa alizuiwa kuongea na viongozi wa
CHADEMA.
Mbowe
amesema hayo juzi katika uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa
CHADEMA katika jimbo la Siha, Elvis Mosi na kudai kuwa Molle hakuwa na
uwezo wa kujenga hoja na ni mtu ambaye amekuwa akijikomba kwa watu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Mollel hajazuiliwa na mtu bali ni Dk. asiye na uwezo, hana uwezo wa kujenga hoja ni mwanaume anajikomba komba kwa watu wa CCM
"....
niwambie watu wangu wa Siha mnapokuwa mnachagua viongozi sisi kama
chama tunawapima kila mwaka, huyu uchaguzi unaokuja ataturudishia jimbo
au atatunyima jimbo?
"Na
kwa vigezo mbalimbali vya chama vilivyofanyika wananchi wa Siha
mshukuru kwa sababu mlikuwa unatuchagulia gunia la misumari bila kujua,
angebaki kwa miaka mingine mitatu kwenye nafasi yake ya Ubunge CHADEMA
wananchi wa Siha mngeichukia" alisema Mbowe
Mbowe
aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha Mollel kujivua uanachama na
kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge jimbo la Siha ni mpango wa Mungu na ni
jambo zuri kwani lingefanya chama hicho kuchukiwa na wananchi.
"Huu
ni mpango wa Mungu aliona wananchi wa Siha nikiwaachia hili gunia la
misumari litakuwa si jambo zuri hivyo akamtia uchizi akaamua kuhama
chama, kwa hiyo hatuna cha kulia kila kitu ni mpango wa Mungu, alijua
kwamba Siha tumejitwisha gunia la misumari"
Post a Comment
karibu kwa maoni