0
Benki Kuu ya Tanzania(BOT) imezifutia leseni za biashara benki tano ambazo ni Covenant Bank for Women(Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera farmers cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited na kuziweka chini ya ufilisi.
Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.
BOT imesema upungufu huu wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.
Hii imetokea ikiwa ni siku moja tu tangu Gavana wa Benki Kuu Tanzania Prof. Beno Ndulu akabidhi ofisi kwa kumaliza muda wake na Gavana mpya kuchukua madaraka.
Soma taarifa yote hapa chini

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top