Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 04 Januari, 2018 amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya
Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum Mhe.
Sam Kutesa ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda.
Pamoja na kupokea barua hiyo Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Mhe. Sam Kutesa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada
ya mazungumzo hayo Mhe. Sam Kutesa amesema Mhe. Rais Museveni amemtumia
Mhe. Rais Magufuli na Watanzania wote salamu za heri ya mwaka mpya na
pia wamezungumzia masuala yahusuyo uhusiano na ushirikiano kati ya
Tanzania na Uganda.
Mhe.
Sam Kutesa amesema Uganda inafurahishwa na kuridhishwa na uhusiano na
ushirikiano mzuri na wa kindugu uliopo kati yake na Tanzania na kwamba
mazungumzo ya leo yalijikita kuuimarisha zaidi kwa manufaa ya wananchi
wa nchi zote mbili.
“Tumezungumza
namna tutakavyoimarisha na kukuza zaidi uhusiano wetu katika maeneo
mbalimbali, kama unavyojua kuna miradi ya maendeleo ya ushirikiano
ukiwemo mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini
Uganda hadi Bandari ya Tanga hapa Tanzania, na miradi mingine na masuala
mbalimbali ya ushirikiano” amesema Mhe. Sam Kutesa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
04 Januari, 201
Post a Comment
karibu kwa maoni