Baada
ya aliyekuwa Waziri Mkuu,Edward Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu
kuonana Rais Magufuli. Hatimae Mbunge wa Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless lema ameibuka na kusema kuwa kiongozi huyo amewakosea
Watanzania kwa kauli aliyoitoa baada ya kutoka Ikulu.
Mh.
Lowassa alipotoka Ikulu baada ya mazungumzo alisema kuwa; “Nimepata
faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na
nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi
nzuri na anahitaji kutiwa moyo, Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni
la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam
hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea
suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na
mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba
tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha
elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya
kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day,” amesema
Lowassa.
Hata
hivyo Lema amemhoji Mh. Lowassa kuwa ni mema gani ameyaona katika
serikali hii, huku akitolea mfano Mbunge wa Singida Mashariki kuwa
anauguza majeraha ya risasi.
“Mh
Lowassa,umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu,mema yapi
umeyaona katika Serikali hii?Wkt Mbunge Lissu bado anauguza majeraha ya
risasi,maiti zinaokotwa,Uchumi unaanguka,Benki zinafungwa ,demokrasia
imekufa Bungeni /Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza,” ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Post a Comment
karibu kwa maoni