0


Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema.

Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema amewataka  wakazi wa mji wake kuhakikisha wanajiaandikisha ili  kupata Vitambulisho vya Taifa zoezi ambalo linaendelea katika mitaa na vijiji mbalimbali.
Mkurugenzi alieleza Kwa Babati uandikishaji  huo ulianza na watumishi  na baada ya hapo unafanyika kwa wananchi kupitia kata zao,hivyo  amewataka watendaji na wenyeviti kutoa ushirikiano kwa NIDA ili wananchi waweze kujitokeza kwa wingi.
Bwana Fwema akizumgumza na WALTER HABARI  ameeleza kuwa katika kata nane zilizopo mjini Babati kata tano tayari zimeshamaliza Usajili huo.
Pia Fwema amezitaja faida ambazo mwananchi atazipata kwa kuwa na Kitambulisho ni pamoja na kutambulika popote pale,kuisaidia seriakali kupata idadi kamili ya wakazi wa eneo husika ,umri wao na kurahisisha serikali kuweza kuwahudumia kwa njia rahisi.
Mkurugenzi wa mjo wa BABATI mkoani Manyara Fortunatus Fwema akionyesha kitambulisho cha Taifa.
Katika hatua nyingine ameipongeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [NIDA] kwa kuendelea kufanya kazi nzuri na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kuwahamasisha wakazi wa mji wa Babati kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha.
Afisa Msajili NIDA wilaya ya Babati ambaye pia ni msimamizi wa shughuli zote za Usajili Mkoa wa Manyara  Emmanueli Joshua  amesema kuwa  zoezi linaendelea vizuri katika awamu ya tatu  ya Usajili ambapo walianza na Magugu Babati vijijini  na awamu ya pili kata ya Nangara ,Mtuka pamoja na Maisaka Babati mjini na kwa sasa wapo katika awamu ya tatu  katika kata ya Babati mjini.
Emmanueli Joshua Msimamizi wa shuguli zote za Usajili [NIDA] Mkoa wa Manyara.

Joshua amesema  licha ya wananchi kuonyesha mwitikio anasisitiza wazidi  kujitokeza kwa wingi zaidi Kusajiliwa kwani ni haki yao ya msingi kupata kitambulisho cha Taifa kwa maendeleo ya Kiuchumi na Usalama.
Amewataka Wale wote ambao bado hawajasajiliwa wafike kwenye ofisi za serikali za mitaa ili kuanza mchakato wa Usajili na wale ambao tayari wamekamilisha kujaza fomu wajitokeze kupiga picha na kuchukuliwa alama za vidole ili kukamilisha zoezi.
Aidha Joshua amesema mwananchi akiwa na Kitambulisho hicho kitamwezesha kupata huduma kijamii kirahisi kama mikopo katika taasisi mbalimbali za Fedha.
Kwa mkoa wa Manyara zoezi hili linaendelea katika maeneo mbalimbali,Babati-Babati mjini, Mbulu-Gehandu,Bargish,Marang,Tlawi na Daudi, Kiteto-Namelock, Hanang-Endasaki na Wareta huku wilaya ya Simanjiro maandalizi yanaendelea baada ya kumaliza maeneo ya Orksemet,Langay na Oldonyogijabe.
Kumbuka kuwa Wanaosajiliwa ni wote wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea,na unapofika katika kituo cha Usajili atatakiwa kuwa na cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la saba au sekondari ,Leseni ya udereva, Bima ya afya, Pasi ya kusafiria.
Amesisitiza kuwa Zoezi hilo ni BURE hivyo Mwananchi hatakiwi kuchangia garama yoyote.
Ameongeza kuwa ili kupata picha nzuri atapaswa kuvaa nguo ambazo haziakisi mwanga, zisizokuwa na maaandishi au nembo ya kampuni.
Naye Afisa Habari wa NIDA  ambaye pia ni Mhamasishaji  katika zoezi la Usajili mkoa wa Manyara na Singida Agnes  Gerald , amesema zoezi hilo ni fursa kwa Wananchi ili waweze kutambuliwa,

NANI NI NANI? YUPO WAPI?ANAFANYA NINI? NA ANAMILIKI NINI KATIKA TAIFA HILI
Hivyo wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi na kusajiliwa kuunga mkono jitihada za serikali kuleta maendeleo kwa wananchi nchini.
Afisa Habari wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [NIDA] Agnes Gerald.

Amesema  kwa sasa wanaenda kwa kasi ili mpaka kufikia mwezi Desemba mwaka 2018 wakamilishe Kusajili nchi nzima huku akitaja mikoa ambayo wameshakamilisha Usajili ni pamoja na Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar visiwani.
Pia amesema   kuwa kwa sasa wanafanya Usajili wa Mkupuo (Mass registration) katika Mikoa mbalimbali nchini  ambapo wanaenda Katika Mitaa kuwafuata Wananchi  kwa lengo la kuwasogezea huduma karibu ili kila mmoja wao aweze kushiriki zoezi hilo hivyo wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi na  kwa wakati mara zoezi linapofika kwenye mitaa/vijiji vyao.
 Hata hivyo ili kuhakikisha wanawafikiwa watu wote kwa njia rahisi NIDA imefanikiwa kuwa na ofisi kila wilaya  nchi nzima.
 Zoezi hilo la Usajili kwa Mkupuo linaendelea katika mikoa  ya Manyara ,Njombe, Mbeya, Songwe, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida, Iringa, Morogoro,Arusha , Kilimanjaro,Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Mikoa  ambayo maandalizi yake yapo katika hatua za mwisho ili kuanza zoezi la Usajili kwa Mkupuo ni pamoja na Tabora, Dodoma, Kagera, Katavi, Bukoba na Kigoma hivyo wananchi wanahimizwa kuandaa viambatanisho muhimu ili kurahisisha zoezi kumalizika kwa wakati litakapoanza katika maeneo yao.

Pia Wananchi wanaweza kuwasiliana na NIDA kwa kupitia njia zifuatazo;
Kwa aliepo Manyara anaweza kufika katika ofisi za kata/mitaa na ofisi za NIDA zilizopo katika wilaya husika au….

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top