
Mwanafunzi Aghata Mwananyau (19), aliyekatisha
masomo akiwa kidato cha nne baada ya kupewa ujauzito, amehukumiwa kifungo cha
miaka sita jela au kulipa faini ya shilingi 300,000.
Msichana huyo aliyekuwa akisoma katika Shule
ya Sekondari ,kangale, katika Mji wa Namanyere, wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa,
aliacha masomo baada ya kupewa ujauzito na Alfa Nestory (20).
Mshtakiwa huyo alishindwa kulipa faini hiyo
ambapo ameanza kutumikia adhabu hiyo.
Juzi aliitwa na upande wa mashtaka kutoa
ushahidi katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, mbele ya Hakimu Ramadhani
Rugemalira ambapo alitoa ushahidi wa uongo akisema aliyempatia ujauzito hakuwa
mshtakiwa Nestory bali alikuwa ‘mmachinga’ aliyetokea Mbeya, tofauti na maelezo
ya awali.
Ndipo Mwendesha Mashtaka, Hakimu Gwelo,
alipomshtaki kwa kutoa ushahidi wa uongo, ambapo jana alifikishwa mahakamani
hapo na alisomewa mashtaka hayo, na alikiri kutenda kosa hilo.
Akitoa hukumu, Hakimu Rugemalira, alisema
amezingatia utetezi wa mshtakiwa kuwa apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mtoto
mchanga mwenye umri wa miezi nane.
Post a Comment
karibu kwa maoni