0


Image result for HOSPITALI YA MRARA BABATI
Hospitali ya wilaya Babati MRARA  Mkoani Manyara imekuwa hospitali yenye kutoa huduma nzuri na bora kwa akina mama/wazazi.
Hospitali ya Mrara iliyopo mjini Babati inahudumia wilaya ya Babati na wilaya jirani ya kondoa mkoani Dodoma.
 Taarifa kutoka kwa Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo imeeleza kuwa  kwa  miaka miwili  2016-2017 katika kitengo cha  huduma ya afya ya uzazi  kumekuwa na mafanikio makubwa kwani  hakujawahi kuripotiwa au kutokea kifo chochote kwa akina mama wakati wa kujifungua katika hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya MRARA Nikodemus Gaudence ameimabia WALTER HABARI kuwa hospitali hiyo imezidi kufanya kazi zake kwa umakini mkubwa ili kuepuka vifo vinavyotokana na uzembe.
Alisema ‘tangu kuanza kutolewa kwa huduma ya wazazi katika hospitali hiyo huduma zimezidi kuwa nzuri kwani miaka miwili sasa haijawahi kutokea vifo vya akina mama waliojifungua hospitalini hapa’.
Dk Nikodemus alisema'Tumekuwa tukijitahidi kutoa huduma bora kadri tunavyoweza  na tunazidi kuboresha,lengo ni kuhakikisha wakina mama waja wazito wanapata huduma bora zaidi,kwa kifupi  tuna kadri miaka miwili sasa tukitoa huduma kwa wajawazito na habari njema hatuwahi kupata kifo hata kimoja ndani ya miaka miwili mfululizo'.Alisisitiza Dk. Nickodemus.
Amesema ni muhimu mama mja mzito akawa na uangalizi  wa karibu kwa kwenda Kliniki kwa kipindi chote cha miezi tisa.
Dk Nickodemus ametoa rai kwa kina mama kuhakikisha kuwa wanajifungulia katika vituo vya afya vilivyopo karibu ili kuepuka matatizo ya kiafya yanayotokana na kujifungua kienyeji.
Pamoja na hayo amewataka Wananchi kuwa na tabia za kupima  afya zao mara kwa mara ili kuweza kuepuka vifo visivyokuwa vya lazima.
‘ Ameeleza kuwa wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukaa na ugonjwa mwilini muda mrefu bila kupima hivyo anapokuja kugundua kuwa ni mgonjwa tayari ugonjwa unakuwa umefikia hatua mbaya zaidi.
Ameendelea kueleza kuwa kwa sasa Hospitali ya mji wa Babati Mrara ina vitengo mbali mbali kama,huduma ya kliniki kwa mama na mtoto,inawahudumia wenye magonjwa ya kifua kikuyu bila malipo,huduma ya macho,kitengo cha huduma ya magonjwa ya Akili,Ushauri Nasaha kwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
Aidha amesema Serikali inaendelea kuonyesha ushirikiano kwa kuendelea kutoa vifaa muhimu vinavyohitajika hospitali ili wananchi wapate huduma bora zenye kukidhi haja ya magonjwa ya wananchi.
Kuhusu wagonjwa wenye kadi za Bima ya afya na wasio na Bima Dk Nikodemus ameeleza kuwa huduma zinatolewa bila ubaguzi kwa watu wote.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top