0
Responsive imageNyota wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Liverpool Mohamed Salah ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2017 katika sherehe za utoaji tuzo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Ghana.
Salah mwenye umri wa miaka 25 amempiku nyota mwenzake wa Liverpool  Sadio Mane raia wa Senegal pamoja na nyota wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon Pierre Emerick Aubameyang ambaye alikuwa anaiwinda tuzo hiyo kwa mara ya pili baada ya kuitwaa mwaka 2015 kwa mara ya kwanza.
Salah ambaye anakuwa mchezaji wa kwanza wa Misri kutwaa tuzo hiyo, alikuwa kwenye kiwango kizuri kwa mwaka 2017 katika klabu yake pamoja timu ya Taifa ya Misri kitu kilichopelekea kuwashinda wapinzani wake hao ambapo amepata alama 625, huku Sadio Mane akipata alama 507 na Aubameyang alama 311.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top