0


Na Gharib Mzinga
Binadamu ameubwa ili aweze kupambana na mazingira yake, Mwenyezi Mungu amempa uwezo wa kujiongeza
ili aweze kuishi vema, Kuna baadhi ya watu wakipata changamoto ndogo tu huanza kuonesha hisia mbaya
Mbele za watu hata kuchukizwa na kila atendewalo, Katika Soka la Afrika kuna baadhi ya mataifa
yamekua na mafanikio makubwa kiasi yanaweza kushiriki michuano mbali mbali ulimwenguni. (Kichuya
unanielewa?)
Hii inatokana na uchu wa wachezaji wake walionao, Nchi za Afrika magharibi zimekua vinara katika kutoa
wachezaji wengi waliotapakaa Katika ligi zote kubwa ulimwenguni, Huko kote wanatafuta riziki, kiasi cha
taifa kua na wigo mpana wa wachezaji, Afrika Magharibi nchi za Nigeria na Ghana huwenda zikawa mfano
bora kwa vijana wake kutokata tamaa na kuchangamkia fursa ya Soka popote. (Kichuya umeelewa?)
Hali hii tofauti na Nchi za Afrika Mashariki, wachezaji wengi wa nchi hizi wamekua watu wa kubweteka,
hawajitumi, Wanalewa sifa huibuka na kuondoka hupotea kabisa, Yupo wapi Said Bahanuzi ?, Poul Nonga,
Ramadhan Singano, Abdulrahman Mussa, Abdulhalim Humoud, Hawa ni mfano tu wa wale waliokuja kwa
mbwembwe lakini kwa sasa hawajulikaniki walipo. (Kichuya unanipata vizuri?)
Pia wapo mmoja mmoja ambao wanajitahidi kua na sifa za kiafrika Magharibi, kama vile Mbwana samata,
Simon msuva, Thomas Ulimwengu, Abdi Banda na Elias Maguli kwa mbali, Hawa ndio wachezaji wachache
katika mamia ya wachezaji wanaopambana na maisha. Mungu awazidishie katika Kutafuta bila kuchoka.
(Shiza unawaona hawa?)
Bila shaka hakuna asiyemjua Victor Moses wa Nigeria na Chelsea, huyu ni mzaliwa wa Nigeria katika jiji la
Lagos, huyu alikua winga Machachari kwa vilabu mbali mbali kama vile Crystal palace, Wigan, westbrom,
Liverpool Huko kote alikua Winga, Alijituma mno Licha ya kutolewa kwa mkopo Mara kadhaa, hakukata
tamaa, Ujio wa Antonio Conte Chelsea umembadilisha kutoka Winga mpaka Mlinzi wa kulia, Hajawai kuwa
bora kama alivyokua sasa akicheza nafasi hiyo. Mchezaji tegemezi Katika club.
Mfumo mpya wa Cattenacio 3-4-3 wa Antonio Conte unamfanya Victor Moses Awe bora na anamsikiliza
mwalimu kwa kila jambo, kwasasa Anategemewa na kikosi cha Nigeria kuwabeba katika Fainali za kombe la
Dunia Mwaka huu. (Shiza unamjua Moses?)
Moses ana mchezaji mwenzake ambaye wanafanana sana tabia na akili, huyu ni Nicholus Gyan wa pale
Simba sc (wekundu wa msimbazi), Huyu alikua Mfungaji Bora huko Ghana katika Club yake ya Dwarf fc
inayoshiriki ligi kuu Ghana, Simba ikamnunua ili kutatua tatizo lao la Ufungaji, Lakini amekua hapati
nafasi sana kama ilivyo kua kwa Victor Moses awali Pale Chelsea, Ujio Wa Masud Djuma na mfumo ule ule
kama wa Victor Moses pale Chelsea, Gyan wamekua hatari akiwa kama mlinzi wa kulia.
Amebdilishwa majukumu kutoka Mshambuliaji mpaka Mlinzi wa kulia, Na ameingia kwenye kikosi bora cha
mapinduzi akiwa kama Mlinzi wa kulia. Sababu kubwa ni Tabia za wachezaji wa Magharibi hufanya jambo
lolote, Gyan na Victor Moses wamezaliwa Nchi jirani kutoka Lagos mpaka Accra kwa ndege zinahitajika
kilometa 456 tu, ndio maana wanafanana Tabia.
Kutoka Accra kwa Gyan mpaka Dar es salaam kilometa 4245, Hapa Gyan anaanzia Wapi kuringa,? Kutoka
Lagos kwa Moses mpaka London kilometa 5020 hapa Moses anaanzia wapi kudeka? Hawa wanatafuta Maisha
Bila kuchoka. (Shiza, Morogoro Mpaka dar kilometa Ngapi vile?) Utanikumbusha.
Shiza kichuya ni Miongoni mwa wachezaji Maridadi mwenye uwezo mzuri, Magazeti ya Bongo yanamwandika
sana kuliko Magazeti ya London yanavyomwandika Victor Moses. Masikini Gyan Nani atakuandika? Wewe
wakuja tu cheza Soka, na usiombe Kuandikwa. Mfumo alioutumia kocha wa Simba sc kule Zanzibar ndio Ule
unaotumiwa na Antonio Conte pale Chelsea, 3-4-3 / 3-5-2 Huu hucheza kwa majukumu zaidi kuliko Namba,
Shiza kichuya unaonekana Kumchukiza sana, Tangu mchezo wa ndanda Kule mtwara.
Haonekani kua na furaha, kwakua mfumo Unafanya akae mbali na Goli, Na yeye amehapa kuwa Mfungaji
bora msimu huu, Hivyo ndoto zake zinaelekea kukatika, Kutokana na kutofurahishwa kwake Masud Djuma
ameliona hilo akaamua kumridhisha kwa kumuweka Namba 9 katika mchezo dhidi ya URA, Lakini hapo
hakufanya kitu chochote alikua mtalii tu, Hali iliyopelekea kufanyiwa madiriko.
Baada ya Mabadiriko Yale Shiza kichuya Alikataa kukaa kwenye Benchi La timu na kwenda kukaa kwa
mashaki huku akionekana kuchukizwa na hali hile!!!. Huyo ndio Shiza kichuya mtoto kutoka Morogoro mji
kasoro Bahari, na klabu haionekani kama ina mpango wa kumuadhibu maana amefanya Uvunjifi wa Nidhamu,
Shiza kichuya hafurahii mfumo wa kocha, Hivyo anaringa, anadeka kujaribu kuonesha hisia zake kwa
vitendo mbele ya washabiki pale Amani.
Kipindi shiza anagomea Benchi, Nicholas Gyan Mshambuliaji wa zamani yupo ndani anakipiga kisawasawa
kama mlinzi wa kulia, Amekubali, Na anapambana, Atamringia Nani? Hawezi katolewa akagomea Benchi
atarudishwa kwao Mapema sana. (Shiza muangalie mwenzako).
Gyan na Victor Moses wakupe funzo kwako na kwa Wachezaji wengine wa kitanzania, Chezeni nafasi yoyote
ambayo utapewa, hakuna kuchagua nafasi, Kwa namna hiyo kuja kufanikiwa litakua suala Humu, Victor
Moses ameshafnikiwa, Gyan amefanikiwa kuwepo kikosi cha kwanza tu, Lakini kwakua amelipata hilo
ataanza kutafuta na Mengine.
Huu ndio utofauti wa wachezaji wa Afrika Mashariki na Afrika Magharibi.
Imeandikwa Na Gharib mzinga.
gharibmzinga@gmail.com

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top