
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametumia ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa Facebook kujibu moja kwa moja maswali aliyoulizwa
na wananchi.
Kupitia mtandao huo jana, Polepole alieleza mafanikio ya CCM yaliyopatikana kwa mwaka 2017.
Katika
kipindi hicho kilichoanza saa 12:00 jioni, Polepole alikuwa akisoma
maswali anayoulizwa na kuyajibu, huku akiviponda vyama vya upinzani
kutokana na madai kuwa wanaohamia chama hicho wanahongwa na kuliingiza
Taifa gharama za uchaguzi.
Akizungumzia
mafanikio ya CCM, alisema yanatokana na mabadiliko makubwa ya muundo
wake kwa kupunguza idadi ya vikao na wajumbe wa ngazi zote.
Katika
mabadiliko hayo, wajumbe wa Halmashauri Kuu wamepunguzwa kutoka 388
hadi 158. Pia kikao hicho kimepunguza idadi ya wajumbe wa Kamati Kuu
kutoka 34 hadi 24.
“Alihama
Nyalandu (Lazaro-aliyekuwa mbunge wa CCM- Singida Kaskazini) kwenda
upinzani wakasifia kuwa demokrasia nzito, nzuri tusimseme ana haki na
tuheshimu mawazo yake lakini Dk Mollel (Godwin-aliyekuwa mbunge wa
Chadema -Siha) kaondoa kurudi CCM wanasema ni gharama ya uchaguzi,”
alisema.
Alisema
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa walihama CCM na kujiunga na Chadema lakini hawakulalamika
“Kwa
kazi nzuri ambayo Rais John Magufuli anafanya sijui kama atabaki mtu,
Dodoma watu wamehamia CCM, huko Tarime chama kinaitwa ACT viongozi wake
wote wamehamia chama tawala, mpaka tukaanza kujiuliza majengo yao
itakuwaje,” alisema.
Alisema hivi sasa chama hicho kina orodha ya makada wa vyama mbalimbali wanaowaelewa.
“Wanatuelewa
maana wanaoongoza kupiga vita ufisadi ni CCM, kama ulisikia mafisadi
hawashikwi, CCM ndio inawashika. wanaoongoza kutoa elimu bure ni CCM na
Serikali yake. Sasa huko upinzani mnafanya nini. upinzani una kazi moja
tu kukosoa,” alisema.
Post a Comment
karibu kwa maoni