Kiongozi
wa upinzani Raila Odinga (NASA) ameapishwa kuwa ‘Rais wa Wananchi’ wa
Kenya licha ya kugomea uchaguzi mkuu wa marudio nchini humo.
Raila Odinga amefika leo katika Uwanja wa Uhuru Park pamoja na viongozi wengine wakuu wa NASA akiwemo Moses Wetangula na Musalia Mudavadi na kujiapisha akishika Biblia.
Aidha,
mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa Chama Cha Wiper hakuwepo wakati
wa kuapishwa kutokana na kuhofia kukamatwa, ambapo Odinga amesema
ataapishwa baadaye.
“Odinga
amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya, hatua ya leo ni kuelekea
kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya, maelekezo mengine mtayapata
baadae,” alisema Odinga baada ya kuapishwa. Awali Raila Odinga
aliiambia kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ‘ si mapinduzi ya
serikali’
Raila
aligomea uchaguzi huo kwa sababu za kusema kuwa tume ya Uchaguzi nchini
humo si ya Uhuru na haki. Uchaguzi huo wa marudio ulikuja baada ya
Mahakama ikiongozwa na Jaji Maraga kutengua Uchaguzi wa awali
uliofanyika 8 Agosti.
Katika
uchaguzi huo wa Oktoba, Rais Kenyatta alitangazwa mshindi akiwa na kura
7.5 milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizokuwa zimepigwa.
Waliojitokeza
kushiriki uchaguzi huo walikuwa 39% kati ya waliojiandikisha kupiga
kura. Kenyatta aliapishwa kuwa Rais wa Kenya baada ya uchaguzi wa
marudio mnamo tarehe 28/11/2017
Post a Comment
karibu kwa maoni