Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za
rambirambi kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma kufuatia kifo cha
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mh. Robert Kisanga kilichotokea tarehe 23,
Januari mwaka huu, Katika Hospitali ya Regence ya Jijini Dar es Salaam
alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo cha Jaji Kisanga
zimethibitishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa John Kahyoza.
Mbali na Mahakama ya Rufaa, Marehemu Jaji
Robert Kisanga alifanya kazi Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Jaji Robert Kisanga aliteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kabla ya
kustaafu mwaka 2008.
Marehemu Jaji Mstaafu Robert Kisanga akihutubia moja ya mkutano enzi za uhai wake. |
Post a Comment
karibu kwa maoni