Kijana mmoja
aliyetambulika kwa jina moja la Boniface mkazi wa Mwananyamala kwa Msisiri
anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa kuiba masanduku ya
kuzikia (majeneza) mawili na kuyaficha nyuma ya choo cha mkazi mwengine wa mtaa
huo
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro,
amesema tukio hilo limetokea kati ya ofisi mbili za kuuza masanduku hayo ambapo
moja ndiyo iliyoibiwa majeneza hayo, ambayo moja ni la mtu mzima na moja likiwa
la mtoto mdogo
Mmiliki
wa masanduku hayo Bi. Judith Carlos amesema masanduku hayo aligundua yapo kwa
jirani yake baada ya kumuahidi mtu atampa elfu 50 iwapo atamsaidia kujua nani
kayachukua, na ndipo baadaye akaambiwa mahali yalipo.
Post a Comment
karibu kwa maoni