Golikipa wa zamani wa Simba, Yanga afariki nchini
Burundi Kipa wa zamani wa Timu za Simba na Yanga na timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa Stars, Ismail Suma amefariki leo akiwa nchini Burundi.
Mbali
na kuzichezea Simba na Yanga, kipa huyo pia aliwahi kuichezea Mbagala
Markets ambayo baadaye ilibadilishwa na kuitwa African Lyon ambayo
aliipandisha daraja mwaka 2009.Mchezaji wa zamani wa aliyecheza na Suma, Patrick Mrope ameiambia RFI Kiswahili kwamba Suma, amefariki dunia akiwa nchini Burundi alikokwenda kutafuta maisha.
“Alikuwa kipa mzuri lakini hakudumu sana kwenye mpira wa Tanzania kutokana na ubabaishaji, tunawasiliana na wadau mbalimbali wa soka ili kusaidia kurudisha mwili wake Tanzania.
Post a Comment
karibu kwa maoni