
Mbunge wa jimbo la Monduli [CHADEMA] mheshimiwa Julius Kalanga ametoa shukrani zake za dhati kwa wananchi wa jimbo lake kufuatia ushirikianio alioupata mwaka uliomalizika 2017 na kuwatakia wote heri ya mwaka mpya na wenye mafanikio 2018.
Kalanga ameimbia WALTER HABARI kuwa mwaka wa 2018 ni mwaka wa kuwatumikia zaidi wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo.
Nawashukuru sana wananchi pamoja viongozi wenzangu wa jimbo la monduli kwa ushirikiano wenu kwangu 2017 katika kutekeleza majukumu yangu ya kusaidiana nanyi kupambana na changamoto mbalimbali zinazotukabili najua haikuwa kazi rahisi km sio ninyi nyote mmesimama nami.
Naamini kwa mwaka 2018 utakuwa mwaka wa mafanikio zaidi tukiwa na mshikamano wa dhati na kuweka maslahi ya monduli mbele. Nawatakia tena baraka za bwana na afya tele. Julius kalanga Mb.
Kalanga [Laigwanan] ni Mbunge wa Monduli kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akimpokea aliekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM kwa Muda mrefu Edward Ngoyai Lowassa aliekihama chama hicho na kwenda CHADEMA ambapo pia aligombea urais mwaka 2015 ambapo kura zake hazikutimia.
Kalanga alimshinda mwenzake wa CCM mtoto wa waziri mkuu wa zamani Edward Sokoine Namelock Sokoine aliepata kura 25,925 huku Julius Kalanga yeye aliibuka mshindi kwa kura 35,024 .
Kalanga alimshinda mwenzake wa CCM mtoto wa waziri mkuu wa zamani Edward Sokoine Namelock Sokoine aliepata kura 25,925 huku Julius Kalanga yeye aliibuka mshindi kwa kura 35,024 .
Post a Comment
karibu kwa maoni