Benki zote nchini
Tanzania na Kampuni za Mawasiliano zinatakiwa kuwa zimejiunga na mfumo wa wa
Kielektroniki wa kukusanya mapato kupitia kituo cha Data kilichopo Kijitonyama
Jijini Dar es Salaam ifikapo Januari 31, 2018 kinyume na hapo Serikali
itanyang’anya Leseni za uendeshaji wa shughuli zao hapa nchini.
Agizo hilo
limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)
alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Benki Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mwaka
2017 zilitungwa Kanuni za Sheria za utawala wa Kodi ambao ulizitaka Benki na
Kampuni za Simu kuwa zimejiunga na Mfumo wa kielektroniki wa kukusanya kodi kati
ya Juni, 2017 hadi Desemba 31, 2017 na mpaka sasa ni Benki 27 tu ambazo
zimetekeleza hatua hiyo ya Kisheria.
‘Nimekutana na
Benki takribani 20 ili kuwasikiliza ni kwanini hawajatekeleza matakwa ya sheria
na katika mjadala huo nimebaini sababu kadhaa zilizosababisha baadhi ya Benki
kuchelewa kuchukua maamuzi, miongoni mwa sababu hizo ni hofu kwa Mamlaka ya
Mapato Tanzania ambayo inaweza kuona miamala na hivyo kuweza kusababisha wizi
wa kimtandao” alieleza Dkt. Mpango.
Sababu nyingine ni
pamoja na Matakwa hayo kuja ghafla hivyo kuhitaji fedha za dharula na Benki
kubwa kama City Bank kuwa na mtandao mkubwa Kimataifa wa nchi takribani 100
hivyo kuwalazimu kuwasiliana na Makao Makuu ya Benki hiyo kabla ya kufanya
Maamuzi.
Hata hivyo kwa kuwa
tayari wamevunja sheria iliyowataka kutekeleza agizo la Serikali kufikia
Desemba 31, 2017, Waziri Mpango amemuagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania, Charles Kichere kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo faini katika
kipindi walichoshindwa kutekeleza sheria.
Dkt. Mpango
amezipongeza Benki zilizotekeleza Sheria ndani ya muda uliowekwa kuwa ni pamoja
na Exim Bank, Benki ya NMB, Benki ya Posta, Amana Benki, CRDB, China Comnercial
Bank, Stanbic na Akiba Commecial Bank na nyingine.
Benki ambazo zipo
katika hatua nzuri ni pamoja na I&M, DCB, DTB, Mkombozi Bank, Maendeleo
Bank wakati Benki ambazo hazijapiga hatua kuwa ni pamoja na Bank of Africa, Yetu
Microfinance Bank, Barclays na Mwanga
Rural community Bank.
Kwa upande wa
Mikopo Chechefu katika Benki, Waziri Mpango ameeleza kuwa hali haikuwa nzuri kwa mwaka 2017 kwa kuwa
Mikopo Chechefu ilifikia asilimia 12 ya mikopo yote ya Sekta ya Benki ambapo
kwa sasa Wadau wa Benki wameona kuna hatua nzuri katika eneo hilo hivyo kufanya
Sekta hiyo kuimarika.
Ameeleza kuwa Benki
Kuu ya Tanzania (BoT) iko imara na Sekta ya Benki kwa sasa ina ukwasi wa
kutosha na si kweli kama mikopo chechefu inaiangusha sekta hiyo.
Post a Comment
karibu kwa maoni