Na Gharib Mzinga
Kila timu ya soka
ulimwenguni inapendelea zaidi kucheza katika uwanja wake wa nyumbani.
Timu nyingi zimekua zikipata matokeo mazuri zinapocheza nyumbani.
Katika
msimu huu wa ligi wa mwaka 2017/2018 umeleta sura tofauti kwa baadhi ya
vilabu vikubwa kushindwa kupata matokeo katika viwanja vidogo dhidi ya
timu ndogo.
Pale Uingereza, Old trafford ni
miongoni mwa viwanja vigumu kupata matokeo, uwanja huu ni mkubwa sana,
unachukua watazamaji 76212, Manchester united ndio bingwa mtetezi wa
Carabao cup au EFL, waliupata ubingwa baada ya kuifunga Southampton 3-2
mwishoni mwa msimu wa mwaka jana.
Manchester
united msimu huu wamevuliwa ubingwa katika hatua ya robo fainali dhidi
ya Briristol city inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza
katika dimba la Ashton gate unaobeba watazamaji 27000.
Arsenal,
hii ni moja wapo ya timu ambazo zinamiliki kiwanja kikubwa cha kisasa
chenye uwezo wa kuingiza watazamaji 60355. Licha ya ugoigoi wao katika
mwendelezo wa ligi lakini Arsenal imekua ngumu kupoteza mchezo katika
uwanja wake wa Emirate.
Arsenal ndio bingwa
mtetezi wa kikombe cha FA, alikishinda kikombe hiko mwishoni mwa msimu
wa mwaka 2016/2017 dhidi ya chelsea kwa ushindi wa 2-1. Arsenal msimu
huu imevuliwa ubingwa wake dhidi ya Nottingham forest inayoshiriki ligi
daraja la kwanza katika kiwanja hafifu cha City ground kinachobeba
watazamaji 30576.
Simba sc hawa ni mabingwa wa
kombe la Azam sports federation cup ASFC. Walichukua msimu wa mwaka
2016/2017 baada ya kuifunga Mbao fc mabao 2-1.
Simba sc msimu
huu wametolewa katika hatua ya awali dhidi ya timu inayoshiriki ligi
daraja la pili ya Green warriors katika dimba la Chamazi Complex.
Somo
linalopatikana hapa ni kwamba, kila timu ya kandanda inaweza kufanya
jambo lolote katika michezo yake, hivyo lazima kila timu iheshimu
mwenzake, na mpira uchezwe bila kubezana, Na timu za madaraja ya chini
zina uwezo wa kufanya vema katika michuano kama hii ya FA hivyo kama nia
itakuwepo na njia itakuwepo pia.
Post a Comment
karibu kwa maoni