0

  Afisa Msajili Mkoa Ndg. Catherine Makuri Bi Catherine Makuri akichambua fomu za wananchi kushoto ili awapatie waingie katika chumba cha Usajili hatua ya pili - uchukuaji alama za kibaiolojia na kulia ni Mwenyekiti Mtaa wa Makungu Ndg. Ramadhani Athumani Assi akimjazisha fomu Ndg. Maria Mtandu Misangi wa mtaa wake mkoani Singida.

Ni katika kata za Uhamaka, Mwankoko na Mtama ambako zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea ambapo wananchi wa kata hizo wamejitokeza kwa wingi Kusajiliwa wakiamini kwa wao kuwa na Vitambulisho vitawasaidia kupata huduma za Kijamii Kirahisi.
Mzee Asumani Said Mkazi wa Kata ya Mwankoko anaeleza kwa yeye kuwa na Kitambulisho cha Taifa atanufaika na huduma za Afya zinazotolewa na Serikali  kwa wazee. 'Nimeamua kuchangamkia fursa hii mapema nisije nikapitwa'
Huku akiendelea kuhudumia wananchi waliofika katika Kata ya Mtama Kusajiliwa, Afisa Msajili Mkoa Ndg. Catherine Makuri ambaye pia ni mratibu wa shughuli za Usajili ngazi ya mkoa - Singida amesema katika mkoa wake wananchi wamejitokeza angalau kwa idadi ya kuridhisha katika baadhi ya vituo vya Usajili ikizingatiwa ni msimu wa kilimo ambapo wengi wanakuwa wako kwenye mashamba yao wakilima  isipokuwa kata chache wananchi wananjitokeza kwa Idadi isiyo ya kuridhisha na wengi kuja majira ya kuanzia Alasiri baada ya kutoka kwenye kilimo. Zoezi la Usajili vitambulisho linaendelea katika wilaya zingine za mkoa wa Singida: Ikungi na Mkalama.  Kwa wilaya ya Manyoni tumeshakamilisha zoezi la Usajili wa mkupuo na kwa Iramba muda si mrefu zoezi litaendelea kwa awamu inayofuatia hivyo wananchi waandae viambatanisho muhimu.

Naye  Mtendaji wa Kata ya Mwankoko Elias Mulamuzi Kayungi  anasema wanajitahidi kutumia mbinu mbalimbali kufikisha ujumbe kwa wananchi ili wajitokeze kushiriki zoezi litakalowawezesha kupata Kitambulisho cha Taifa. Ndg. Kayungi anatoa rai  kwa 'Hakikisheni Mnatumia fursa hii Adhimu Kujisajili kwani wakati huu NIDA wanaendesha Usajili wa Mkupuo ambapo  huduma imesogezwa karibu na makazi yenu iwapo hamtajitokeza itawagharimu kufika kwenye ofisi zao wilayani'.
 
  Wananchi wa Kitongoji cha Ikusi B wakiwa waejitokeza Kusajiliwa bila kuzuiliwa na mvua iliyokuwa inaendelea kunnyesha. Wazee nao walikuwemo kama anavyoonekana na mkongojo wake lengo likiwa kuhakikisha anakuwa na Kitambulisho cha Taifa.
 Bi catarina Fidel akiwa anapatiwa huduma ya Usajili hatua ya pili ya uchukuaji alama za kibaiolojia katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
  Wananchi wa Kata ya Mtamaa mkoani Singida katika foleni kuelekea kuchukuliwa alama za kibaiolojia (Picha , Saini na Alama za vidole)
      
Umati Wananchi wa Kata ya Mwankoko wake kwa waume wakiwa waejitokeza Kusajiliwa katika kituo cha Usajili Mwankoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top