0

Katibu Tawala (DAS) wilaya ya Ikungi mkoani Singida Bi. Winifrida akitoa maelekezo kwa msaidizi wake wa pili kushoto kuhakikisha anatoa ushirikiano kwa Maafisa wa NIDA kwa  kuhakikisha watendaji Kata na Wenyeviti wa vijiji Wanahamasisha wananchi wao wajitokeze Kusajiliwa. Wa tatu kushoto ni  Afisa Msajjili Wilaya (RRO) ya Ikungi mkoani Singida Bi Agnes Mtei na Afisa Msajili Bi. Doris Niyukuri wa Ofisi ya Usajili NIDA - Ikungi.

Ameyasema hayo Afisa Msajjili Wilaya (RRO) ya Ikungi mkoani Singida  Bi Agnes Mtei alipokuwa anatembelea vituo vya Usajili kuangalia maendeleo ya zoezi  linalofanyika wilayani hapo chini ya Uratibu wa ofisi ya Usajili ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa anayoisimamia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya - Ikungi.

Bi. Mtei amesema kwa sasa wameshakamilisha tarafa 2 kati ya 4 zilizoko kwenye wilaya hiyo  ambazo ni: Ikungi yenye kata za (Ikungi, Nkiwa, Isuna, Unyahati, Mangonye na Dugunyi) na Sepuka yenye kata za Sepuka, Mwaru, Mtunduru, Igombwe, Mgungira,  Iyombo na Irisia  ambapo wananchi wameweza kufikiwa na zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa katika kata wanazoishi.

Aidha Bi. Mtei ameeleza kwa sasa zoezi linaendelea katika tarafa ya Ihanja katika kata za Puma, Kituntu, Ihanja, Isokena Iglanson, Muhintiri, Makilawa, Minyuhe  na inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii ndipo wataendelea katika tarafa ya mwisho iliyosalia ya Mongaa na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kutumia fursa hiyo kwani huduma zimesogezwa karibu katika kata na mitaa wanakoishi ili iwe rahisi kwao kushiriki.

Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa inaendesha zoezi la Usajili wa mkupuo katika mikoa takribani 16 ambayo ni pamoja na Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha , Mbeya, Njombe, Songwe, Ruvuma, Iringa, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mwanza, Lindi, Mtwara na Morogoro huku ikijiandaa kuingia katika mikoa ya Tabora, Dododma, Kigoma na Kagera ambapo kwa mikoa ya Dar es Salaam,  Pwani, Tanga na Zanzibar zoezi la Usajili wa mkupuo limekamilika hivyo wananchi wanaendelea kupata huduma mbalimbali katika ofisi ya Usajili Vitambulisho vya Taifa katika mikoa hiyo.
 
Afisa Msajjili Wilaya (RRO) Ikungi mkoani Singida  Bi Agnes Mtei akitafuata fomu ya Usajili wa Maombi ya Kitambulisho cha Taifa ambayo Mzee Fadhili Mtandu wa miaka 82 mkazi wa wilya ya Ikungi aliijaza ili aingie kwenye hatua ya pili ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia kwa kutumia mashine za BVR.


Afisa Mtendaji Kata ya Ihanja Ndg. Juma kifuda akimjazia fomu mwananchi Hassan Alli Mohamed aliyefika kituo cha Usajili Vitambulisho vya Taifa akitokea kijiji cha Ihanja.
Afisa Msajili Wilaya (RRO) ya Ikungi mkoani Singida  Bi Agnes Mtei akikagua maendeleo ya zoezi katika kituo cha Usajili Kata ya Ihanja, Kijiji cha Chungu kitongoji cha Mburu. Kulia ni Afisa Msajili Msaidizi Bi Julita Ikoti Nkungu akiendelea Kusajili mwananchi  aliye mbele yake ambaye hayuko pichani.

Wananchi wa Kijiji cha Chungu wakiendelea Kusajiliwa katika kituo cha Usajili Chungu kilichoko wilaya ya Ikungi mkoani Singida.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top