Chama cha mapinduzi [Ccm]
mkoa wa Manyara kinatarajia kuvuna wanachama zaidi ya mia tatu [300] kuelekea
maazimisho ya miaka 41 ya chama hicho jumatatu Feb 5 kesho.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa umoja wa wanawake wa
Tanzania [UWT] Mkoa wa Manyara Haines Munisi wakati akizungumza na wanawake wa
umoja huo katika kata ya Bonga na Babati mjini.
Bi Haines amesema kuwa katika kusheherekea miaka ya kuzaliwa
chama hicho kila mwaka wanafanya shughuli mbalimbali ambapo kwa mwaka huu
wanaazimisha kwa kukagua na kuweka miapaka kataika maeneo ya Chama,kupanda miti
na kuwatembelea watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wagonjwa waliolazwa
Hospitalini,watoto yatima na kuwapatia misaada mbalimbali.
![]() |
Katibu wa umoja wa wanawake mkoa wa Manyara UWT Haines Munisi |
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Ccm UVCCM Taifa Kheri James akiwa mkoani Manyara ijumaa Februari 2 .2018 katika kambi maalum ya
vijana kata ya Kiru Babati vijijni aliwakabidhi
kadi wanachama wapya 130 waliokihama chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA].
Kheri James akizungumza na vijana hao aliwapongeza kwa
kurejea Ccm na kuwahidi kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kuwaondolea vijana
changamoto ya ajira inayowakabili
Post a Comment
karibu kwa maoni