Chama cha
mapinduzi tarehe tano februari kinasheherekea miaka 41 tangu kuanzishwa kwake
mwaka 1977.
Katika
kuelekea sherehe hizo umoja wa wanawake
Tanzania UWT mkoa wa Manyara wakiongozwa na Katibu wa umoja huo Haines Munis
wamesema wanasheherekea miaka hiyo kwa kuwatembelea wagonjwa na kupanda miti
ambapo leo wametembelea kituo cha Afya Bonga Halmashauri ya mji wa Babati na
kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa na wahudumu wa Kituo hicho ikiwemo
sabuni.
Msaidizi wa Mganga
mkuu mfawidhi wa kituo cha afya Bonga
Dk. Onesmo Ole Kimboria amesema zipo changamoto nyingi zinazokikabili kituo
hicho ikiwemo kukosa usafiri wa kuhamisha mgonjwa aliyezidiwa,chumba cha
X-Ray,chumba cha kuhifadhia maiti,uhaba wa vyumba vya kulaza wagonjwa.
Dk.Ole
Kimboria ameomba halmashauri pamoja na baraza la madiwani kutatua changamoto
hizo ili kuweza kutoa huduma bora za afya.
Pia Wakina
mama kutoka UWT Manyara waliwatembelea wanafunzi kuwatembela watoto wenye
mahitaji muhimu katika shule ya msingi Bonga na kuwapa msaada wa madaftari na
kalamu.
Watoto hao
ambao wameonekana wakiwa na huzuni muda mwingi huku wakitokwa na machozi kwa
kile kinachoonekana kuwakumbuka wazazi wao waliowatoka duniani, wamewafanya
wakina mama walofika kuwatembea nao kutokwa na machozi.
Hata hivyo
watoto hao wameahidi kusoma kwa bidii na kuwasaidia wale wasiojiweza.
watoa
machozi wakina mama hao waliofika darasani wakati wakifundishwa jumuiya tatu za
chama hiko kinaendelea na shuguli mbalimbali za kijamii.
Kwa upande
mwingine umoja wa wanawake wa Ccm Tanzania mkoani Manyara umeahidi kurudi tena
shuleni hapo na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo mavazi kwa watoto hao,vifaa
vya shule na kuwapeleka baadhi yao katika shule zenye hosteli.
Post a Comment
karibu kwa maoni