
Naibu
Waziri wa Mambo ya ndani ametangaza leo kwamba kuanzia tarehe 1 Machi
2018 kuwa utaanza ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kwamba kila
gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu
tatu.
Akizungumza
jana na wanahabari, Mh. Masauni alisema kwamba Wamiliki wa magari
madogo wanatakiwa kupeleka magari yao katika vituo vya polisi ili
yafanyiwe Ukaguzi kama yanastahili kuendelea kuwepo barabarani.
Aidha
Mh. Masauni amewaonya maaskari kuhusu zoezi hilo kwa kuwaambia kwamba
"Askari yoyote atakayetumia nafasi yake kutoa stika ya gari bila
kulifanyia ukaguzi na ilihali halina vigezo vya kupewa stika nataka
niwaambie kuwa huu si wakati wake, zama zimebadilika".
Pamoja
na hayo Mh. Masauni aliongeza kwamba "Nataka madereva wa pikipiki
ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala
ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja".
Kwa
upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania,
Fortunatus Musilimu alisema katika Ukaguzi wa magari madogo utakaoanza
mwezi ujao, mtu atakaekiuka na kukataa kupeleka gari lake kufanyiwa
ukaguzi atakamatwa na sheria itachukua mkondo wake.
Post a Comment
karibu kwa maoni