Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssekibogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe amefariki.
Bw Balaam Barugahara, ambaye ni promota, anasema kuwa Radio alifariki dunia Alhamisi majira ya saa kumi na mbili asubuhi.Radio alifariki katika hospitali ya Case mjini Kampala ambako alikuwa amelazwa baada ya kuripotiwa kupigwa hadi kupoteza fahamu kwenye kilabu cha pombe cha De Bar, kilichopo katika mji wa Entebbe wiki iliyopita.
"Utawala wa hospitali ya Case wanasikitika kutangaza kifo cha Moses Ssekibogo alias Moze Radio leo tarehe 1 Februari 2018 saa kumi na mbili asubuhi," ilisoma sehemu ya taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Case kuhusiana na kifo hicho.
Hii inakuja saa chache baada ya rais Museveni kuchangia Shilingi milioni 30m, pesa za Uganda kwa ajili ya matibabu yake.
Wiki iliyopita, polisi walisema kuwa waliwakamata watu watano kwa ajili ya kuisaidia katika uchunguzi wa polisi juu ya kisa cha kumpiga Radio.
Post a Comment
karibu kwa maoni