"Ushuru
ni ugonjwa , kila sehemu ushuru, ushuru , wabunge wenu wameshapitisha
sheria. Mtu akiwa na chini ya tani moja ya mzigo asitozwe ushuru. Kwenye
minada kulikuwa hata na ushuru wa kwato za ng'ombe, hivi unaweza
kulizuia ling'ombe lisiwe na kwato?, “ amehoji Rais Magufuli.
Ametoa
kauli hiyo leo Machi 10, 2018 wakati wa uzinduzi wa barabara ya
kilometa 45 kutoka Uyovu hadi Bwanga wilayani Bukombe, mkoani Geita
iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Barabara hiyo ilikamilika ujenzi wake Oktoba, 2017 na imejengwa kwa fedha za ndani kwa ajili ya asilimia 100.
Huku
akizungumza mara kwa mara Kisukumu na kuwafanya wananchi waliohudhuria
uzinduzi huo wa barabara kuangua kicheko, Magufuli pia alikemea kundi la
watu aliodai kuwa hawapendezwi na kasi ya mafanikio katika sekta
mbalimbali.
"Kuna
watu hawapendi kuona amani hii tuliyonayo. Dhana halisi ya kutunza
amani, amani ni kitu muhimu, hata mitume walihubiri amani, Yesu
aliwaambia nawaachieni amani, kwa hiyo nawaambia amani tuliyonayo
imejengwa na Mwalimu (Julius Nyerere), amekuja Mwinyi (Ali Hassan) na
akaja KIkwete (Jakaya) pia ameitunza amani,” amesema.
"Tuwazuie
dhahabu, tutengeneze reli kutoka Dar ,Dodoma, mpaka Lusumo na iwe ya
umeme, nani anafurahi? Nani afurahi kuona barabara za lami zikijengwa?.”
Post a Comment
karibu kwa maoni