Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la James Eric Davis Jr
anatuhumiwa kuwapiga risasi wazazi wake hao wakiwa katika bweni analoishi, siku
moja baada ya kwenda hospitali kutokana na suala linalohusiana na matumizi
wa dawa za kulevya.
Wazazi hao ni Diva Davis, 47,
na James Erick Davis Sr, 48,
ambao inaelezwa kuwa walipigwa risasi na mtoto wao wakiwa ghorofa ya
nne ya Ukumbi wa Campbell
ulioko ndani ya chuo alichokuwa anasoma ambapo ndipo bweni lake lilikuwepo.
Mwanasheria wa Jimbo la Illinois aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter
kuwa familia hiyo inaishi eneo la Chicago ambapo baba wa
mtoto huyo alikuwa ni Askari Polisi
hadi mauti ilipomfika leo.
Post a Comment
karibu kwa maoni