Maofisa
wawili nchini Burundi wamehukumiwa kwenda jela baada ya Rais wa nchi
hiyo, Pierre Nkurunziza kuwashutumu ‘kuchezewa vibaya’ wakati wa mechi
ya mpira wa miguu waliyoiandaa.
Rais
Pierre Nkurunziza ambaye ni 'Mlokole' wa Kanisa la Evangelical
Christian amekuwa akitumia muda wake mwingi kusafiri na Timu yake ya
Haleluya FC ndani ya Burundi kwa ajili ya kushiriki mechi mbalimbali.
Inadaiwa kuwa Februari 3, Rais huyu na timu yake walicheza na Timu ya mji wa Kaskazini mwa Kiremba.
Kama
kawaida, upande wa timu pinzani ulikuwa ukifahamu kuwa unacheza na rais
wa nchi na kukubaliana kuwa mchezo utakaochezwa utakuwa mwepesi, na
hata kuweza kumruhusu Nkurunziza kufunga goli.
Lakini
kutokana na Timu ya Kiremba kuwa na wachezaji wengi ambao ni wakimbizi
kutoka Congo ambao hawakujua kama wanacheza na rais wa Burundi, walikuwa
“wakimshambulia mara kwa mara anapokuwa na mpira na kumwangusha mara
kadhaa", shuhuda aliwaeleza AFP.
Waliohukumiwa
kwenda jela, Juzi Alhamisi ni pamoja na Mratibu wa Kiremba Cyriaque
Nkezabahizi na msaidizi wake, Michel Mutama, kwa mujibu wa shirika la
habari.
Post a Comment
karibu kwa maoni