Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema Tanzania hakuna
tishio lolote kuhusu watu kupotea au kuuawa kama inavyoelezwa na baadhi ya watu
na kusema kuwa Wizara yake inapambana kuhakikisha watu na mali zao wako salama.
Waziri mwigulu Nchemba alisema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na kudai kuwa miili ya watu ambayo imekuwa ikiokotwa baharini si miili ya Watanzania kwani kama ingekuwa miili ya Watanzania hivyo basi familia zao zingekuwa zinasikika kizipiga kelele kuhusu ndugu zao hao kupotea.
Aidha Waziri Mwigulu Nchemba ametaka ajenda za watu zisigeuke kuwa siasa na kusema kuwa ajenda za siasa zifanywe kwenye siasa na si maisha ya watu pia Mwigulu Nchemba amedai kuwa katika matukio rasmi ambayo wao waliyapata ni kuhusu kutekwa kwa watoto Arusha.

Post a Comment
karibu kwa maoni