Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 9,
2018 ameonya watu wanaopanga kuandamana akidai kuwa huu sio muda wa maandamano
bali ni muda wa kujenga taifa.
Rais
Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanapenda kuona Tanzania ikiwa
na migogoro kila siku na wanafurahi kuona watu wanaandamana mabarabarani.
“Wapo watu wangependa nchi hii kila siku tuwe
na migogoro, Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli, wangependa
kila siku tupo mabarabarani tunaandamana.
Watu wao wanahamia huku wao
wanataka wabaki wanaandamana kule, nimeshasema ngoja waandamane wataniona, kama
kuna baba zao wamewatuma watakwenda kuwasimulia vizuri,“amesema Rais Magufuli leo Machi 9,
2018 kwenye uzinduzi wa tawi la benki ya CRDB mjini Chato.
Kauli hiyo
ya Rais Magufuli imekuja wakati kukiwa na taarifa zikizagaa mitandaoni kuwa
kuna watu wanapanga maandamano yasiyo rasmi.
Kwa upande
mwingine Rais Magufuli amewataka Watanzania kufanya kazi na kuwa wavumilivu kwa
kipindi hiki cha mwanzo hadi tutakapofika kwenye nchi ya asali.
Wakati huo
huo Rais John Magufuli amesema licha ya kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei anakaribia kustaafu ameahidi kumpatia nafasi
katika Serikali ya Awamu ya Tano.
“Kimei wewe ustaafu tu lakini nasema nafasi bado zipo.
Muda wako unamalizika CRDB lakini Serikalini bado unaweza kufanya kazi ndani ya
Serikali bado upo na ninakuahidi asilimia 100,” amesema Rais Magufuli.
Post a Comment
karibu kwa maoni