Shirikisho la soka nchini (TFF) kupitia kwa bodi ya ligi (TPLB) limetangaza mabadiliko ya ratiba ya ligi ikiwa ni ndani ya saa 24 tangu litoe ratiba mpya iliyojumuisha viporo vya Simba na Yanga.
Leo
mchezo namba 199 wa Ligi Kuu kati ya Mbeya City na Yanga uliopangwa
kufanyika Mei 1, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya umebadilishwa na sasa utapangiwa tarehe nyingine.
Taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza kuwa uamuzi wa kuipangia tarehe nyingine mechi hiyo ni kukidhi matakwa ya Kanuni inayotaka nafasi kati ya mechi moja na nyingine isiwe chini ya angalau saa 72.
Kwa mujibu wa ratiba, Yanga itakuwa na mechi dhidi ya Simba itakayofanyika Aprili 29, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo itakuwa ni vigumu kusafiri na kwenda kucheza huko Mbeya ndani ya saa 72.

Post a Comment
karibu kwa maoni