Waziri
wa Mambo ya ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na
harakati za kutengeneza taswira mbaya za serikali badala yake kuwa na
mitazamo chanya.
Aliyasema
hayo katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara
(CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum, Ester Mmasi.
Alisema
wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani
yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.
“Nilishawahi
kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu..majina yangu
yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya
ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” alisema Dk Mwigulu.
Alisisitiza
kuwa wanafunzi wengi kwa sasa wamekuwa wakiitafuta taswira mbaya ya
serikali bila kuangalia masuala mengine yanayopaswa kuungwa mkono.
“Kuwa
kijana mwema chuoni sio kwa kuwa kimya Bali kuwa na mitazamo chanya
naukiona mwanazuoni anabisha jambo jema ujue kuna kasoro,” alisema
Post a Comment
karibu kwa maoni