Amesema
siku hiyo washtakiwa watasaini bondi ya Sh20 milioni na wakiwa huru
ndipo utaratibu wa kukata rufaa wa upande wa mashtaka utafanyika.
“Nikitoa dhamana wakati washtakiwa hawapo haina maana zoezi zima lisimame.Leo washtakiwa hawajafikishwa mahakamani na nimetoa masharti ya dhamana, hivyo kutoa dhamana na washtakiwa wakiwa bado hawajasaini ilo zoezi bado halijakamilika.
“Hivyo kwenye hatua ya sasa ni mapema mno kwa upande wa mashtaka kuwasilisha hoja za kukata rufaa wakati bado mchakato haujakamilika.
“Mahakama inatoa remove order waje mahakamani April 3,2018 na wadhamini wao ili waje kukamilisha masharti ya dhamana.” Amesema Hakimu Mashauri.

Kufuatia
uamuzi huo, viongozi hao watakula Sikukuu ya Pasaka wakiwa mahabusu.
Sikukuu hiyo inasherehekewa kuanzia kesho hadi Jumatatu.
Awali, Hakimu Mashauri alieleza dhamana kwa washtakiwa hao iko wazi, jambo ambalo lilipingwa na upande wa Serikali.
Washtakiwa
hao walitakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati
ya dhamana ya Sh20 milioni na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao ama
wa vijiji au mtaa, ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.
Hakimu alisema kwa asiyeridhika na uamuzi huo ana haki ya kukata rufaa.
Katika
mvutano wa kisheria, mmoja wa mawakili wa viongozi hao, Peter Kibatala
alipinga taarifa ya rufaa iliyotolewa na wakili wa Serikali.
Kibatala
aliiomba mahakama kutekeleza amri yake ya dhamana kwa kuwasainisha
washtakiwa bondi ya Sh20 milioni kila mmoja katika tarehe ambayo inaona
inafaa na baada ya hapo ndipo ipokee taarifa ya Serikali ya kukata
rufaa.
Wakili
wa Serikali, Faraja Nchimbi alidai kuwa hilo ni suala la kisheria kwa
kuwa taarifa ya rufaa ikishawasilishwa mahakamani na kupokewa, mahakama
husika itakuwa imefungwa mikono kuongea chochote kuhusiana na taarifa
hiyo kwa maelezo kuwa itakuwa imeingia katika kumbukumbu za mahakama.
Post a Comment
karibu kwa maoni