Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.
Wakili Nchimbi amedai kuwa kosa la kwanza ni kufanya mkusanyiko ama maandamano yasiyo na uhalali.
Kwa
pamoja wanadaiwa Februari 16, 2018 wakiwa barabara ya Mkwajuni kwa
pamoja walikusanyika kwa lengo la kutekeleza mkusanyiko ili watu
waliokuwepo eneo hilo waogope kuona maandamano ya kuvunja amani.
Kosa
la pili ni kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali, ambapo
linawakabili washtakiwa wote wakidaiwa kutenda kosa hilo Februari
16,2018 Barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni.
Kwa
pamoja wanadaiwa wakiwa na watu wengine 12 ambao hawajafikishwa
mahakamani wakiwa katika maandamano na mkusanyiko wa vurugu waligoma
kutii amri ya kusambaratika na kuvunja mkusanyiko huo uliosababisha
kifo cha Akwilana Akwiline na majeraha kwa maofisa wa Polisi.
Wakili Nchimbi amedai kuwa kosa jingine ni kuhamasisha chuki kwa wanajamii isivyo halali, ambalo linamkabili Mbowe.
Inadaiwa
Februari 16, 2018 akiwa viwanja vya Buibui Kinondoni DSM akihutubia
wakazi wa maeneo hayo na DSM alitoa matamshi ambayo yangesababisha chuki
kwa Jamii.
Pia
kosa jingine linalomkabili Mbowe ni uchochezi na kusababisha chuki
katika jamii, ambapo inadaiwa amelitenda Februari 16,2018.
Inadaiwa akiwa Uwanja wa Buibui Kinondoni DSM akihutubia wakazi wa DSM alitoa matamshi ambayo yangepelekea chuki katika Jamii.
Pia
Mbowe anakabiliwa na kosa jingine la uchochezi wa uasi, ambapo inadaiwa
amelitenda Februari 16,2018 katika viwanja vya Buibui Kinondoni DSM.
Inadaiwa
akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya uongozi uliopo
madarakani alitoa maneno ambayo ni wazi yangesababisha uasi.
Pia
kosa jingine linalomkabili Mbowe ni uchochezi wa uasi, ambapo inadaiwa
amelitenda Februari 16,2018 katika viwanja vya Buibui, Kinondoni DSM.
Inadaiwa
akihutubia mkutano wa hadhara alitoa matamshi ambayo yangepandikiza
chuki na dharau kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya uongozi uliopo
madarakani.
Kosa
la saba linamkabili Mbowe ambalo ni ushawishi wa utendekaji wa kosa la
jinai, ambalo amelitenda Februari 16, 2018 maeneo ya Buibui Kinondoni
DSM.
Inadaiwa Mbowe akiwa amejumuika na watu wengine aliwashawishi wakazi wa maeneo hayo na DSM kutenda kosa.
Katika kosa la 8, Wakili Nchimbi amedai linamkabili Msigwa ambalo ni kushawishi raia kutenda kosa la jinai.
Msigwa
anadaiwa ametenda kosa hilo Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui
Kinondoni DSM, ambapo aliwashawishi wakazi wa maeneo hayo na DSM
kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana ambapo Wakili
Nchimbi amedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarehe kwa
ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
Hata
hivyo, Wakili Nchimbi aliwasilisha maombi kwa mahakama hiyo ili
washtakiwa wanyimwe dhamana kwa sababu ya usalama wa umma wa Watanzania.
Post a Comment
karibu kwa maoni