Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, amesema Benki hiyo imeridhishwa na
utekelzaji wa miradi ya nishati hapa nchini kwani inachochea mageuzi katika
maisha ya wananchi .
Akizungumza mara baada ya kuwasili Mkoani
Dodoma na kutembelea kituo cha kupoza
umeme cha Zuzu, mkoani Dodoma, amesema kuwa
benki hiyo inatambua na kupongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.
Dkt.
Adesina ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme ni mkakati wa
Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme
kwa wananchi wake na umelenga pia kupunguza tatizo la upatikanaji wa umeme
katika nchi jirani zinazopakana na Tanzania ikiwemo Burundi na Kenya.
Alisema
kuwa katika kuhakikisha mpango huo wa kupeleka umeme huo na kuunganisha na nchi
jirani, Benki yake imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 75 kufanikisha
mradi huo wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 220.
"Umeme
ni jambo muhimu sana katika maendeleo ni sawa na damu katika mwili wa binadamu,
ukiwa na damu mwilini unakuwa na hai kama huna unakufa! kwa hiyo uchumi bila
umeme wa uhakika hauwezi kushamiri" alisisitiza Dkt. Adesina
Aliahidi
kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza maendeleo
ambapo hivi sasa Benki yake iko katika mazungumzo na Serikali ili mkopo nafuu
wa dola za Marekani milioni 165 uweze kupatikana kwa ajili ya kujenga mradi wa
nishati ya umeme katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa nchi.
"Vile
vile tutawasilisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Benki yetu ili kiasi cha dola
za Marekani milioni 45 kinachoombwa na Serikali kwa ajili ya kujenga mradi wa
umeme unaotokana na joto ardhi uweze kupatikana ili kuboresha na kuwa na umeme
wa uhakika nchini kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya viwanda nchini"
alisema Dkt. Adesina
Alisema
kuwa kwa ujumla Benki yake katika kipindi cha miaka miwili ijayo (2018/2019 na
2019/2020) Benki yake itatoa kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.5 katika
sekta ya umeme na kueleza matumaini yake kwamba hatua hiyo itawawezesha
wazalishaji mali wadogo, wa kati na wakubwa kuzalisha bidhaa na mali mbalimbali
na hivyo kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.
Kituo
cha kupoza umeme zuzu ni sehemu ya mradi wa umeme unaonufaisha mikoa ya Iringa,
Dodoma, Singida na Shinyanga ambapo vijiji zaidi ya 121 vimeshanufaika na
maradi huo wa uzalishaji na usambazaji
wa umeme kwa mikoa husika.
Alisema
kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki
yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji
mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara,
kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na
uendelezaji wa rasilimali watu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa
Serikali ya Tanzania inashukuru kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshirika
mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na kusaidia Serikali katika uwekezaji
mkubwa unaogusa nyanja mbalimbali
ikiwemo nishati na miundo mbinu mingine kama barabara.
Aliongeza
kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuwalketea wananchi
maendeleo ya kweli kwa kuwa hiyo ndio dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati Mhe. Mheshimiwa Subira Mgalu amesema kuwa Benki
hiyo ni mshirika wa kweli katika sekta ya nishati na imewezesha kufanikiwa kwa
miradi mbalimbali ya umeme ukiwemo ule unaoinifaisha mikoa ya Iringa, Singida,
Dodoma, Shinyanga na Dodoma.
Miradi
inayotekelezwa hapa nchini kwa sasa
kupitia ufadhili wa Benki ya AfDB imefikia zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo
uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya
barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali
pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
Ushirikiano
wa AfDB na Tanzania ulianza tangu mwaka 1971 na mpaka sasa benki hiyo imeipatia
Tanzania kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.6, karibu shilingi trilioni 8 za
Tanzania.
Rais wa AfDB
yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Dkt.
John Pombe Magufuli.
Post a Comment
karibu kwa maoni