0
Moja kati ya stori zinazochukua headlines kwa sasa ni kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Misri anayeichezea Liverpool ya England Mohamed Salah kuweka rekodi ya kihistoria ndani ya Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018.

Salah baada ya kuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu England EPL akiwa na Liverpool leo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya tatu ya mchezaji bora wa mwezi March wa Ligi Kuu England EPL.

Mohamed Salah kwa msimu wa 2017/2018 pekee amefanikiwa kushinda tuzo hiyo mara tatu akianzia mwezi November, February na March hivyo kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tatu leo kunamfanya kuwa mchezaji pekee EPL kuwahi kushinda tuzo hiyo mara tatu kwa msimu mmoja.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top