Bunge
limeiagiza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kutosita kufuta chama
chochote cha siasa kinachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendesheji
wa vyama vya siasa nchini.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa
amesema hayo bungeni leo Jumatano aprili 4, wakati akitoa maoni ya
kamati yake kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, mwaka
2018/19.
“Kamati
inashauri na kusisitiza kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
ihakikishe kunakuwa na usimamizi wa karibu kwa kufuatilia na kuchunguza
mienendo inayoharibu sifa na vigezo vya vyama vya siasa nchini na kwamba
Msajili asisite kufuta usajili wa chama chochote cha siasa
kitakachokiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya
siasa,” inasema hotuba hiyo ya Kamati.
Pamoja
na mambo mengine, kamati hiyo imeishauri ofisi hiyo ifanye ufuatiliaji
na na ukaguzi wa matumizi ya ruzuku kwa vyama vya siasa ili kuhakikisha
kuwa matumizi ya ruzuku hizo yanazingatia madhumuni yaliyokusudiwa.
“Ikibainika
ruzuku hizo zinatumika tofauti na madhumuni hayo, chama husika kisipewe
ruzuku ili kutoa fundisho kwa vyama vyote kuzingatia matumizi stahiki
ya fedha za wananchi,” alisema Mchengerwa.
Post a Comment
karibu kwa maoni